Searching...
Jumanne, 10 Desemba 2013

MISA YA KUMUAGA MZEE NELSON MADIBA MANDELA INAENDELEA HIVI SASA

Watch Nelson Mandela's memorial service live
HUU NDIO UWANJA WA SOCCER CITY UNAOTUMIKA KATIKA MISA YA KUMUAGA MANDELA HIVI SASA.
Misa ya kitaifa ya wafu kumuaga Hayati Nelson Mandela, inaendelea mjini Johannesburg Afrika Kusini.
Rais wa Marekani Barack Obama na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon watakuwa miongoni mwa viongozi wa dunia watakaohutubia muhadhara huo.

Zaidi ya Viongozi wakuu wa nchi 90 wanaohudhuria misa ya wafu ya Mandela,kati yao ni pamoja na:-

 
RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA.
 
KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA BWANA BAN KI MOON.
 
RAIS WA CUBA RAUL CASTRO.
RAIS WA UFARANSA FRANCOIS HOLLANDE.
WAZIRI MKUU WA UINGEREZA DAVID CAMEROON.
RAIS WA BRAZIL DILMA ROUSSEFF.
RAIS WA ZIMBABWE ROBERT MUGABE.
RAIS WA TANZANIA JAKAYA KIKWETE.
Viongozi hao pia watahutubia wananchi sawa na wajukuu wanne wa Mandela .
Maelfu ya watu wamehudhuria misa hiyo katika uwanja wa FNB.
Afrika Kusini imeandaa shughuli mbali mbali za kumuenzi Mandela kabla ya siku ya kuzikwa kwake nchini Afrika Kusini siku ya Jumapili.
Misa ya leo ni moja ya mikusanyiko mikubwa ya viongozi wa kimataifa iliyoshuhudiwa nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.
Viongozi wengine Watakaohudhuria misa ya wafu ya Mandela:

Watu wengi wamekaidi hali mbaya ya hewa ambapo mvua kubwa imenyesha huku wakikusanyika uwanjani humo wakisubiri kwa muda mrefu kabla ya misa hiyo kuanza muda mfupi uliopita.
Waliohudhuria misa hiyo wamesemekana kuwa wenye furaha wakiimba nyimbo na kutaja jina la Mandela kwa shangwe unaweza kudhani ni mkutano wa kisiasa.
Misa hiyo itafanyika katika uwanja ambako Nelson Mandela alionekana kwa mara ya mwisho hadharani.
Misa hiyo itaonyeshwa kwenye skrini kubwa nje ya uwanja ili kuzuia msongamano wa watu.
Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95 na kwa wengi yeye ni shujaa na mkombozi wa Afrika Kusini.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!