Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kocha wa makipa wa Simba, marehemu
James Kisaka likiingizwa kwenye basi la klabu hiyo, baada ya kutolewa
heshima za mwisho katika misa iliyofanyika katika Kanisa la Muhimbili,
Dar es Salaam. Marehemu Kisaka atasafirishwa kwenda kwao wilayani
Muheza, Tanga kwa mazishi yatakayofanyika kesho.
Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mumewe
Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio',
(kushoto) akijadiliana jambo na baadhi ya wachezaji wa soka waliokwenda
kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka.
Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akifarijiana na mtoto wa
pili wa marehemu Kisaka, Boniface baada ya kutoa heshima za mwisho.
Ndugu wa karibu wa marehemu Kisaka akilia alipokuwa akitoa heshima za mwisho
Mtoto wa mwisho wa marehemu Kisaka, Christopher akitoa heshima za mwisho
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania ambaye
pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania
Limited, Juma Pinto (kushoto), akisalimiana na Mwenyekiti wa zamani wa
Klabu ya Simba, Hassan Dalali.
Wachezaji soka wa zamani wakijadiliana jambo nje ya Kanisa la Muhimbili
walipokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James
Kisaka. Kutoka kushoto ni Madaraka Selemani, Peter Tino, Khamis Kinye,
Bakari Malima na Thomas Kipese.
Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio', (kushoto)
akijadiliana jambo na baadhi ya wachezaji wa soka waliokwenda kutoa
heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka.
Benny Kisaka ambaye ni mdogo wa marehemu James Kisaka akisoma wasifu wa marehemu kakake
Msanii wa filamu Jacob Steven JB akitoa heshima za mwisho
Mchezaji wa zamani wa Simba Malota Soma akitoa heshima za mwisho kwa mchezaji mwenzie marehemu Kisaka.
Mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula akitoa heshima za mwisho
Benny Kisaka ambaye ni mdogo wa marehemu, akitoa taarisha ya usafiri wa kwenda kwenye msiba baada ya kutoa heshima za mwisho.
0 comments:
Chapisha Maoni