Askari
wa Kikosi cha Zima moto na Uokoaji Wakiwa wamepanda juu ya Mnara wa
Simu Uliopo Ubungo Jijini Dar Es Salaam Muda mfupi uliopita kwaajili ya
kumuokoa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Hassan Ambaye
alipanda juu ya mnara huo kwa lengo la kufikisha Ujumbe wa kutaka
kuonana na Raisi Kikwete ili aweze kumwelezea kwa kile anachodai kuwa
jeshi la polisi lilimbambikia kesi na hatimaye kuhukumiwa kifungo cha
Miaka 6 kwenda jela
Askari
wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiendelea na zoezi la kumuokoa
Kijana Hassan kwaajili ya kutojirusha kutoka Juu ya Mnara wa Simu Muda
mfupi uliopita Ubungo Jijini Dar Es Salaam Leo
Hapa akishushwa na askari wa Kikosi Cha Zimamoto na Uokoaji
Hapa
Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji akiwa amemuweka begani na
Kushuka nae chini Mara baada ya kufanikiwa Kumshika vizuri kwaajili ya
kumteremsha chini bila kupata madhara
Kijana
aliyefahamika kwa jina moja la Hassan akiongea na waandishi wa habari
mara baada ya kushushwa juu ya Mnara wa Simu na Askari wa Kikosi cha
Zimamoto na Uokoaji muda mfupi uliopita Ubungo jijini Dar
Tukio likiendelea huku wakazi wa jiji la Dar Wakiendelea kushuhudia.
0 comments:
Chapisha Maoni