ALIYEKUWA KOCHA WA YANGA ERNST BRANDTS.
Taarifa za uhakika na za kuaminika kutoka klabu ya Yanga zilizotufikia hivi punde zinasema kocha wa klabu hiyo iliyofungwa magoli 3-1 na watani wao wa jadi wekundu wa msimbazi simba Ernst Brandts amefutwa kazi rasmi leo.
taarifa zaidi zinasema kikao cha kamati ya mashindano kilichokaa jana ndicho kilichoibuka na maamuzi hayo mazito ambapo hata mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji ameridhia uamuzi huo.
cha kushangaza zaidi ni kwamba ameambiwa aendelee kufundisha hadi hapo timu itakapopata kocha mpya ndani ya mwezi mmoja kutoka leo.
FELIX MINZIRO KOCHA MSAIDIZI WA YANGA AMBAYE NAYE KIBARUA CHAKE KIPO MATATANI
makocha wengine wawili mzawa Minziro na Siwa wamewekwa kiporo japo dalili zinaonyesha wazi kwamba hata wao ajira zao zipo mashakani
0 comments:
Chapisha Maoni