Rais
wa kwanza Mzalendo na Mpigania Uhuru wa Afrika Kusini Mzee Nelson
Mandela ‘Madiba’ akiwa ameshikilia viatu vyake ambavyo aliviacha
nyumbani kwa Mzee Nsilo Swai alipoingia Tanzania kwa mara ya kwanza
mwaka 1962 akitokea Afrika Kusini ili kuanza harakati za ukombozi.
Mzee
Mandela aliahidi kuvichukua viatu hivyo pindi atakaporejea Tanzania
lakini katika safari hiyo ndipo alipoishia mikononi mwa makaburu wa
Afrika Kusini na kumfunga kwa miaka 27. Viatu
hivyo vilihifadhiwa hadi alipotoka na kukabidhiwa kwa Mandela na mjane
wa Mzee Nsilo Swai, Bi Vicky Nsilo Swai (pichani kulia) Desemba 12,1995 Mandela alipotoka gerezani na hatimaye kuwa Rais wa kwanza Mweusi wa Afrika Kusini.
0 comments:
Chapisha Maoni