Basi la Mohamed linalofanya safari zake kutoka Mwanza kuelekea Bukoba limeacha njia na kuvamia mashamba yaliyopo pembezoni mwa barabara asubuhi ya leo. |
Kwa mujibu wa mpenyezaji wa taarifa hizi ambaye alikuwa akipishana na basi hilo amesema kuwa hakuna abiria yeyote alipoteza uhai wala aliyejeruhiwa zaidi ya abiria kadhaa kujawa hofu. |
Mpaka mpenyezaji wa taarifa hii anatoka eneo la tukio matairi ya basi hilo yalikuwa yamezama kwenye tope huku juhudi za kuliondosha basi hilo kurejea barabarani zikifanyika. |
0 comments:
Chapisha Maoni