Akizungumza
 kwa niaba ya kamati ya utendaji, mjumbe wa kamati ya utendaji Joseph 
Itangare amesema wamemsimamisha mwenyekiti kutokana na kufanya maamuzi 
yake binafsi bila kushirikisha kamati ya utendaji ikiwemo kutoitisha 
vikao vya kamati ya utendaji kwa mujibu wa Ibara ya 31 (1)ya katiba ya 
simba.
Kingine
 alichosema Itangare ni ‘vilevile mwenyekiti huyo amesaini mkataba wa 
kukiuuza kipindi cha Simba tv bila kushirikisha kamati ya utendaji’
Hii picha hapa juu 
ni Mzee Kinesi ambae namkariri akisema ‘kwa sasa lazima twende kikatiba,
 Mwenyekiti kama hayupo ngazi inayofatia inapanda juu na tunachagua 
Mjumbe mwingine ili kukaa kwenye nafasi iliyobakia, kwa muda huu wa 
matayarisho ya mkutano mkuu ujao mimi nitakaimu kama Mwenyekiti wa Simba
 na Swed atakaimu kama makamu Mwenyekiti’
Kwenye
 sentensi nyingine, Kinesi amesema ‘Mwenyekiti tumemsimamisha lakini 
tusubiri maamuzi ya mkutano mkuu ambao utafanyika kwa ajili ya 
marekebisho ya katiba, kuna mengine yamekiukwa hivyo yatawasilishwa 
kwenye mkutano mkuu tarehe 1 December’
‘Kutokana
 na timu yetu kutofanya vizuri, tumeamua kwamba benchi la ufundi 
tulifumue ili tulijenge upya, sasa litaongozwa na kocha aliekua na Gor 
MahiaZDRAVOK
 LOGARUSIC amekubali kuja na ataanza mazoezi tarehe 2 December na kwa 
pamoja tumekubaliana ndie atakua kocha mkuu, pia tumekubaliana Matola 
ndio awe msaidizi wake kwa muda, hatumuondoi Simba B moja kwa moja 
kuhofia kutetereka’
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni