RAIS WA KENYA UHURU KENYATA
Mahakama ya Kimataifa ya kushughulikia kesi za
uhalifu wa kivita, ICC imetengua uamuzi wake wa awali uliomruhusu Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta kutohudhuria baadhi ya vikao vya kesi ya uhalifu
wa kivita inayomkabili.
Mahakama hiyo sasa imesema kuwa ni lazima Bwana
Kenyatta afike binafsi mbele ya mahakama hiyo kusikiliza kesi yake na
ushahidi unaotolewa dhidi yake.
FATOU BENSOUDA,MWENDESHA MAHAKAMA MKUU ICC
Mahakama hiyo imesema kama sheria inavyotaka, Bwana Kenyatta lazima
binafsi ahudhurie vikao vya kesi inayomkabili. Imesema maombi yoyote ya
baadaye ya kutaka asihudhurie baadhi ya vikao vya kesi hiyo,
yatafikiriwa kutoka na msingi wa suala linaloombewa ruhusa hiyo.
Mahakama hiyo imefikia uamuzi kwamba hukumu
iliyotolewa katika rufaa ya tarehe 25 Oktoba 2013 ya Mwendesha mashitaka
dhidi ya William Samoei Ruto na Joshua Arap Sang, imetoa taarifa mpya
muhimu ambayo inahalalisha kuangaliwa upya kwa suala la kesi hiyo.
Mahakama ya Rufaa ya ICC imehitimisha kuwa
Mahakama ina hiyari kwa mujibu wa kifungu namba 63(1), kinachosema kuwa
"mtuhumiwa ni lazima awepo mahakamani wakati kesi inayomkabili
ikiendeshwa", lakini hiyari hiyo imewekewa kikomo. Mahakama ya Rufaa
imetoa uamuzi kwamba mtuhumiwa kutofika mahakamani, inaruhusiwa tu pale
panapokuwa na sababu maalum na za kipekee, na lazima sababu hizo ziwe
zinakidhi hoja kwa mtuhumiwa kutofika mahakamani hapo.Imeendelea kusema
kwamba uamuzi wa kama mtuhumiwa aruhusiwe kutohudhuria sehemu ya vikao
vya kesi yake lazima uzingatie hali halisi ya ombi la mtuhumiwa.
0 comments:
Chapisha Maoni