Askari polisi pamoja na askari wa vikosi maalumu zanzibar wakihesabu meno ya Tembo yapatayo 1023 yenye jumla ya uzito wa kilo 1922 ikiwa ni uzito na idadi kubwa ya meno ya tembo kukamatwa hapa nchini
Meno haya ya Tembo yalikamatwa jana jumatano katika bandari ya zanzibar,ambapo idadi ya meno hayo ni sawa na Tembo 512
Kamanda wa Kikosi cha Polisi Bandarini Zanzibar akiongoza Operesheni wa kukagua magunia yaliokuwa na Pembe za Tembo yaliokamatwa katika bandari hiyo leo yakiwa katika harakati ya kusafirishwa nje ya Nchi kupitia bandari hiyo, zoezi hilo limefanywa chini ya Jeshi la Polisi Bandari Kikosi cha KMKM, yalikuwa katika Kontena la futi 40.
Askari
wa jeshi la Polisi wakitoa Pembe za Tembo katika magunia wakati wa
zoezi hilo leo asubuhi katika bandari ya Malindi Zanzibar.
Magunia
haya yakiwa na shehena na makombe ya pwani wakati katikati yakiwa na
viroba vya Pembe za Tembo ambayo yakiwa yamehifadhiwa katika Kontena
likiwa tayari kusafirishwa nje ya Nchi, limegunduliwa katika bandari ya
Zanzibar leo asubuhi.
Baadhi
ya Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari ya Malindi Zanzibar
zikisubiri kuhesabiwa kupata idadi kamili na thamani yake na uzito kwa
ujumla.
Operesheni ikiendelea kuhesabu Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari ya
Zanzibar wakiweka hesabu sawa kuhakikisha hesabu iliokamilika na kupata
thamani yake halisi.
Zikipimwa uzito kujuwa uzito wake kila gunia likipimwa kupata uzito wake wote.
Zikipimwa uzito kujuwa uzito wake kila gunia likipimwa kupata uzito wake wote.
0 comments:
Chapisha Maoni