Mgeni Rasmi katika
Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa
PPF,Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa (katikati) akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa Nembo Mpya ya PPF iliyoambatana na Tovuti
Mpya ya PPF.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa PPF,Dk. Aggrey Mlimuka na
kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio.
Hivi ndivyo inavyoonekana Nembo Mpya ya PPF.
Mgeni Rasmi
katika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa Pensheni
wa PPF,Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa akitoa hotuba yake wakati
akifungua mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano
wa AICC,jijini Arusha kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo Oktoba 2
mpaka Oktoba 5,2013.
Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF,Dk. Aggrey
Mlimuka akitoa hotuba yake mapema leo asubuhi wakati wa ufunguzi
wa Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa
PPF unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini
Arusha.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio akizungumza leo kwenye
Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,unaofanyika leo
kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Meneja
Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Lulu Mengele akifafanua jambo juu
ya Muonekano wa Logo Mpya ya Mfuko huo iliyozinduliwa Rasmi leo kwenye
Ukumbu wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wakuu wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii nchini,Daudi Msangi
akitoa shukrani kwa mgeni rasmi na kwa wadau wote kwa ujumla kwa
kuitika kwao wito kwenye Mkutano huo.
Bw. Bonda Nkinga akitoa Ushuhuda wake wake mbele ya
Wanachana na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa
Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza kuwasaidia watoto zake kusoma kupitia Fao la elimu.
Kijana Peter
William Mulokozi ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha Tano katika Shule
ya Sekondari ya Mzumbe akitoa ushuhuda wake mbele ya Wanachana na Wadau
wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza
kumsaidia yeye kusoma,mara baada ya Baba yake kupoteza maisha
ghafla.PPF ambao ni Mfuko pekee unaotoa fao la Elimu nchini endapo
Mwanachama anakuwa amefariki akiwa kwenye ajira.PPF imeweza kumsaidia
kijana huyu kusoma mpaka hapo alipofikia.
Kijana
Pascalia Nsatto ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha sita katika Shule ya
Sekondari ya Kimataifa ya Moshi akitoa ushuhuda wake mbele ya Wanachana
na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF
ilivyoweza kumsaidia yeye kusoma,mara baada ya Wazazi wake wote wawili
kupoteza maisha.
Ilikuwa ni
huzuni tu wakati vijana hao wakitoa ushuhuda wao wa namna walivyoweza
kusaidiwa kimasomo na Mfuko wa Pensheni wa PPF pindi walipoondokewa na
wazazi wao.
Waheshimiwa
Wabunge wakifatilia kwa umakini Hotuba ya Mgeni Rasmi katika Mkutano wa
23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Waziri wa
Fedha,Dkt William Mgimwa (hayupo pichani) alipokuwa akifungua.
Viongozi kutoka Chama cha Wafanyakazi.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara mbali mbali ndani ya Mfuko wa Pensheni wa PPF wakifatilia mkutano huo.
Mgeni Rasmi
katika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF,Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa akitoa Tuzo wa
Washindi mbali mbali wa PPF wanaoongoza kwa kuwasilisha michango yao kwa
wakati.
Mrisho Mpoto akitoa burudani.
Burudani ya Ngoma za asili.
Mkutanoni.
Picha ya pamoja.
0 comments:
Chapisha Maoni