Mwenyekiti wa
CCM mkoa wa IringaNdugu Jesca Msambatavangu akiwaongoza viongozi wa
vyama vya ukombozi mara tu walipowasili mkoani Iringa kwa ziara ya siku
moja ya kutembelea chuo cha Ihemi, Viongozi hao wapo nchini kuhudhuria
mkutano wa sita wa Makatibu wakuu wa vyama vya Ukombozi utakaofanyika
tarehe 9,Septemba 2013 jijini Dar es salaam.
Viongozi
mbalimbali kutoka vyama vya ukombozi wakifurahia ngoma za asili wakati
walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa nduli tayari kwa ziara ya siku
moja kukitembelea chuo cha Ihemi.
Viongozi kutoka
vyama vya Ukombozi Afrika wakionyesha ishara ya mshikamano wakati Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwakaribisha rasmi kwenye chuo
cha Ihemi mkoani Iringa.
Katibu Mkuu wa
CCM ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa kuwakaribisha
viongozi wa Vyama vya Ukombozi katika chuo cha Ihemi.
Viongozi kutoka
vyama mbali mbali vya ukombozi Afrika pamoja na marafiki wa vyama hivyo
kutoka China wakiangalia eneo la Chuo cha Ihemi walipotembelea leo
mkoani Iringa.
Katibu Mkuu wa
Chama cha SWAPO Ndugu Nangolo Mbumba akizungumza na waandishi wa habari
baada ya kutembelea eneo ambalo chuo cha Viongozi Vijana kitajengwa na
kusema Tanzania ni nchi ambayo imefanya kazi kubwa kulikomboa bara la
Afrika.
Sehemu ya eneo la chuo cha Ihemi mkoani Iringa ambapo kitakapojengwa chuo kikubwa cha Uongozi kwa Vijana.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na Katibu Mkuu wa chama cha
Flerimo cha Msumbiji Ndugu Filipe Paumda pamoja na wageni wengine kutoka
vyama vya ukombozi Afrika na chama rafiki cha kikomunisti cha China
wakitembelea maeneo mbali mbali kwenye chuo cha Ihemi ambapo kitajengwa
chuo cha Viongozi Vijana .
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi akiwaonyesha viongozi kutoka vyama vya Ukombozi Afrika
,ukubwa na uzuri wa eneo ambalo chuo cha Viongozi Vijana Afrika
kitajengwa.
Mratibu wa Chuo
cha Ihemi Ndugu Lucas Kisasa akifafanua baadhi ya mambo muhimu ya chuo
hicho kwa Naibu Waziri katika Idara ya Kimataifa kutoka china Ndugu Ai
Ping .
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akizungmza na Billy Masetlha na
Obed Bapela kutoka chama cha ANC cha Afrika Kusini wakati wa ziara yao
kwenye chuo cha Ihemi mkoani Iringa.
Viongozi mbali
mbali wa vyama vya Ukombozi wakiagana na viongozi wa CCM mkoa wa Iringa
baada ya kukamilisha ziara yao ya siku moja ya kutembelea chuo cha Ihemi
mkoani hapo.
0 comments:
Chapisha Maoni