Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk Emmanuel Nchimbi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa barabara ya lami ambayo
inamaliziwa kujengwa yenye urefu wa mita 600 iliyopo katika Kata ya Mjini,
Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Barabara hiyo imegharimu zaidi ya Sh75
milioni. Dk Nchimbi yupo mjini Songea kwa ziara ya siku tano akikagua pamoja na
kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo jimboni mwake.
Sehemu
ya mamia ya wananchi wa Kata ya Mjini, Manispaa ya Songea wakiwa tayari kwa
kumsikiliza Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Dk Nchimbi baada ya kuzindua barabara
yenye kiwango cha lami yenye urefu wa mita 600 ambayo imegharimu zaidi ya Sh75
milioni, pia mbunge huyo ameweka jiwe la msingi katika ofisi ya Kata ya Mateka.
Dk Nchimbi katika ziara yake ya siku tano jimboni humo, pia anatarajiwa
kuzindua ujenzi wa mabweni ya sekondari pamoja na nyumba za walimu.
Dereva
wa bodaboda (pikpiki) akinyanyuliwa juu kwa furaha na wananchi waliohudhuria
mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi baada ya Mbunge wao
kuyajibu maswali yake. Mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika
Kata ya Mjini, Manispaa ya Songea walipewa nafasi ya kumuuliza mbunge wao
maswali mbalimbali. Dk Nchimbi baada ya kuzindua barabara yenye kiwango cha
lami yenye urefu wa mita 600 ambayo imegharimu zaidi ya Sh75 milioni, pia
mbunge huyo aliweka jiwe la msingi katika ofisi ya Kata ya Mateka. Dk Nchimbi
katika ziara yake ya siku tano jimboni humo, pia anatarajiwa kuzindua ujenzi wa
mabweni ya sekondari pamoja na nyumba za walimu. Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akilifungua jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Mateka iliyopo mjini Songea mkoani Ruvuma. Dk Nchimbi pia alizindua barabara yenye kiwango cha lami yenye urefu wa mita 600 ambayo imegharimu zaidi ya Sh75 milioni iliyopo katika Kata ya Mjini, Manispaa ya Songea. Dk Nchimbi yupo mjini Songea katika ziara ya siku tano ya kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.
Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na mamia ya wananchi wa Kata ya Mateka, Mjini
Songea baada ya kuizindua barabara yenye kiwango cha lami yenye urefu wa mita
600 ambayo imegharimu zaidi ya Sh75 milioni iliyopo katika Kata ya Mjini na
baadaye kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya Kata ya Mateka. Dk Nchimbi katika
ziara yake ya siku tano jimboni humo, pia anatarajiwa kuzindua ujenzi wa
mabweni ya sekondari pamoja na nyumba za walimu.
0 comments:
Chapisha Maoni