Mtaalamu wa Upishi wa Bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Calvin Nkya (kulia) akitoa maelezo kuhusu utendaji wa kiwanda cha bia cha Dar es Salaam,wakati maofisa wa kikosi cha polisi cha usalama barabarani, walipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi. TBL ilidhamini maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyomalizika hivi karibuni.
Meneja Uhusiano wa TBL, Editha Mushi akiwakaribisha baadhi ya maofisa wa kikike kutembelea kiwanda hicho.
Editha Mushi akitoa maelezo kwa baadhi ya maofisa
Mmoja wa maofisa wa kikosi cha usalama barabarani akijitambulisha
Consolata Adamu wa TBL, akielezea kuhusu kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt
Nkya akitoa maelezo kuhusu utendaji wa kiwanda cha Bia cha Dar es Salaam.
Maofisa wakitembezwa katika moja ya idara ya utengenezaji bia
Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Ibrahim Mwamakula (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo, wakati maofisa wa kikosi cha polisi cha usalama barabarani, walipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Dar es Salaam kujua utendaji wake. TBL hivi karibuni ilidhamini maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyomalizika hivi karibuni.
Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Mrakibu wa Polisi, Meloe Buzema akipokea zawadi kutoka kwa Kilindo
Maofisa wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TBL, baada ya kumaliza ziara.
0 comments:
Chapisha Maoni