Searching...
Alhamisi, 17 Oktoba 2013

HUU NDIO UMATI WA WATU ULIOMZIKA MAMA YAKE UFOO SARO

Mtoto wa mwandishi na mtangazaji wa kituo cha ITV,Ufoo Saro,Alvis Anthery akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la marehemu Bibi yake Anastazia Saro aliyezikwa jana katika makaburi ya kanisa la Urara wilayani Hai.
Umati wa waombolezaji waliojitikeza katika kuaga mwili wa marehemu Anastazia Saro aliyezikwa katika makaburi ya kanisa la Urara wilayani Hai.
Msemaji wa familia ya Saro,Allelio Swai akitoa maelezo ya familia wakati wa ibada ya kumuombea marehemu Anastazia Saro.
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Anastazia Saro likiwekwa kaburini.
Mkuu wa jimbo la Hai,Aminirabi Swai akiongoza ibada ya maziko katika makaburi ya kanisa hilo na kisha kuweka shada la maua katika kaburi la marehemu Anastazia Saro.
mwakilishi wa serikali katika maziko ya marehemu Anastazia Saro ,mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga akiweka shada la Maua katika kaburi.
Mtoto Alvis Anthery akiweka shada la maua katika kaburi la Bibi yake marehemu Anastazia Saro.
(picha na Dixon Busagaga)

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!