ARSENE WENGER-KOCHA ARSENAL.
'Hakuna mazungumzo yoyote juu ya kuongeza mkataba wangu hapa Arsenal,na mwisho wa siku nitaamua nini cha kufanya.unamhukumu kocha kutokana na kile alichokifanya na klabu...alisema Wenger
Timu ya Arsenal jumamosi hii watashuka dimbani kumenyana na timu ya Sunderland kwenye uwanja wa mwangaza "Stadium of Light" wakiwa na pengo kubwa katika safu ya ushambuliaji baada ya washambuliaji wake kukabiliwa na majeruhi.
Wenger anaonekana kujiamini zaidi baada ya kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Mesut 'Ozil ambapo amekua akimsifia kwamba ataisaidia sana timu kunyakua makombe mengi msimu huu.
JE NDOTO ZA WENGER ZITATIMIA?
0 comments:
Chapisha Maoni