MHESHIMIWA EDWARD LOWASA.
Bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea na vikao vyake ikiwa ni mkutano wa 12 kikao cha sita,asubuhi hii katika kipindi cha maswali na majibu limepatwa na msuko suko baada ya mbunge mmoja kuitaka serikali kutoa tamko kuhusu nini msimamo wao kuhusu kuruhusu wananchi wa kigoma,Rukwa na Katavi kujitengenezea mvua zao za asili(kichawi) ili kuinusuru nchi na tatizo la ukame ili kuweza kuendeleza kilimo hapa nchini.
akijibu swali hilo naibu waziri wa kilimo mheshimiwa Mheshimiwa Adam Kigoma Malima amesema kamwe serikali haitaruhusu mambo ya kienyeji ambayo hayajafanyiwa utafiti.
Hata hivyo jibu hilo la serikali lilipelekea wabunge wengi kusimama kuomba kuuliza maswali ya nyongeza ambapo wabunge wengi walitaka kujua kama kuna mambo ya kienyeji lakini yenye manufaa kwanini yasiruhusiwe? hapo ndipo waziri wa kilimo aliposimama na kusema hakuna mvua yoyote ya kienyeji,huo ni uongo ambao mwisho wa siku unaweza kuleta uvunjifu wa amani pale utakaporuhusu na watu wajiandae na kilimo alafu isiponyesha nani atawalipa hao wakulima fidia kwa kuwadanganya.
Sinema hiyo ya aina yake haikuishia hapo tu,mbunge mwingine alisimama na kuiuliza serikali kuhusu ile mvua ya Lowasa imeishia wapi?
Swali hilo lilijibiwa na waziri wa mazingira Dr. Terezya P.L. Huvisa,ambapo alisema hakuna mvua ya Lowasa,Rukwa,Katavi wala kigoma tatizo ni mabadiliko ya hali ya hewa duniani.
Majibu hayo yalileta tofauti ya majibu ya serikali pale waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uratibu na bunge mheshimiwa William Lukuvi aliposimama na kusema Mvua ya Lowasa ipo,na ndio maana kipindi kile akiwa waziri mkuu aliwaleta wataalamu kutoka Malesia ila serikali ikakosa fedha...."sasa waheshimiwa mawaziri mnatuchanganya humu ndani,waziri wa mazingira anasema Mvua ya Lowasa haipo,Waziri wa nchi (Lukuvi) unasema mvua ipo,sasa tumuamini nani? sasa nawaomba mkakae mawaziri mnaohusika mjadiliane mje mtuambie jibu moja ambalo ndilo tutakaloliamini kwamba ndilo jibu la serikali"alihoji mwenyekiti wa bunge mheshimiwa Jenista Mhagama.
Mvutano huo ulimlazimu mheshimiwa Lowasa kusimama na kutolea tamko mvutano huo...."Mheshimiwa Mwenyekiti,nimesimama hapa kutoa tamko kwamba jibu alilolitoa mheshimiwa Lukuvi (kwamba mvua ya malesia ipo) ndilo jibu la ukweli,ahsante mheshimiwa mwenyekiti..Alifunguka Mheshimiwa Lowasa.
0 comments:
Chapisha Maoni