MWANADASHOSTI anayejipanga kurejea
kwenye gemu la Bongo Fleva kwa kishindo, Rehema Chalamila ‘Ray C’
amefunguka ya moyoni akisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kupona madhara
ya madawa ya kulevya bila kupata matatizo mengine ya kiafya huku
akifafanua suala la kuokoka.
Mwanamuziki
huyo alisema kuwa katika kipindi chote cha kupigana na madawa ya
kulevya zaidi ya miaka mitatu iliyopita, alipitia mengi magumu lakini
kikubwa ni kwamba hivi karibuni alipima na kujikuta yupo salama na hana
Ukimwi.
Kuhusu suala la kuokoka, Ray C alisema
ukweli ni kwamba mwanzoni alikuwa Mkatoliki lakini hivi karibuni
alibatizwa na maji mengi katika Kanisa la Sloam lililopo Mbezi-Beach na
kuungana na mama yake anayesali kwenye kanisa hilo.
“Namshukuru Mungu nimepona, sina tatizo
la kiafya kama Ukimwi. Kuhusu kuokoka, mimi sijaokoka, Nilibatizwa na
maji mengi. Napenda mahubiri ya Sloam.
Nimeungana na mama yangu
anayesali kanisani hapo ndiyo maana watu wanatafsiri kuwa nimeokoka.“Watu
wakisikia mtu anasema ameokoka wanatafuta vitu ili kukujaribu.
Kweli
mimi sijaokoka lakini mahubiri yananiweka huru na nakuwa na amani
zaidi,” alisema Ray C