Kichwa cha habari peke yake
kinatisha,jaribu kufikiria kama hili linawezekana katika dunia hii??? amini
usiamini bibie Betty Mbereko mwenye umri wa miaka 40 amefikia maamuzi ya
kuolewa na mwanaye wa kumzaa mwenyewe,ambaye ni mtoto wa kwanza wa uzao wake.
Mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la
Farai Mbereko mwenye umri wa miaka 23 inasemekana amekua akiwa na mahusiano ya
kimapenzi ya siri na mama yake miaka mitatu iliyopita mara tu baada ya baba
yake kufariki dunia.
Taarifa za uhakika zinasema mpaka
sasa mama huyo anao ujauzito wa miezi sita ambapo ameonelea ni vyema tu
wakaweka wazi mahusiano yao na kuoana rasmi badala ya kuolewa na mdogo wa
marehemu mume wake kama mila yao inavyotaka.
Mama Betty ameiambia mahakama ya
kijiji chao kwamba ameanza mahusiano ya kimapenzi na mwanaye miaka mitatu
iliyopita..."nimeanza mapenzi na mwanagu miaka mitatu iliyopita,nimepata
shida sana kumsomesha mwanangu baada ya baba yake kufariki,hakuna mtu yoyote
amenisaidia,sasa leo hii nafurahia matunda ya jasho langu nyie
mnanishtaki...!!! tafadhali niacheni nifurahie matunda yangu."alifunguka
mama Betty Mbereko.
Kwa upande wake mume mtoto bwana
Farai amesema yupo tayari kumuoa mama yake na atalipa mahari yaliyosalia ambayo
baba yake alikua anadaiwa kabla hajafariki ”ninajua baba yangu alifariki kabla
hajamaliza kulipa mahari ya mama,kwa sasa najiandaa kupeleka malipo hayo ya
mahari yaliyosalia,”alifunguka mume mtoto.
“ni vyema tukaweka wazi mahusiano
yangu na mama,kwasababu nataka jamii ijue kwamba mimi ndio nimempa mimba mama
yangu,vinginevyo najua watamyanyapaa sanaI
Msemaji wa
kijiji hicho amesema kamwe hawawezi kukubali jambo hilo likubalike kwani itakua
ni laana kwa kijiji chetu,.."kama ingekua ni zamani hawa watu wangepaswa
kuuwawa,lakini kwa sasa hatuwezi kwasababu tunaogopa polisi na mahakama"alimalizia
msemaji huyo wa kijiji.
0 comments:
Chapisha Maoni