ROY HODGSON.
Meneja wa timu ya Uingereza Roy Hodgson, amesema
aliridhika na walivyocheza wachezaji wake walipojitosa katika michuano
ya kuwania kombe la dunia.
England ilimaliza mchezo kwa sare tasa dhidi ya Ukraine kwenye mechi iliyochezwa mjini Kiev
Kikosi cha Hodgson kinasalia juu
katika kikundi cha H na kitafuzu ikiwa kitashinda mechi zao mbili za
kufuzu dhidi ya Montenegro na Poland zitakazochezwa katika uwanja wa
Wembley.
Baadhi ya mechi ambayo walisema ilikosa
msisimuko na ambayo ilichezwa mbele ya mashabiki 70,000, meneja huyo wa
England alisema, "kabla ya mchezo, hisia waliyokuwa nayo wengi ni kwamba
matokeo ya sare yoyote hayatakuwa mabaya.''
GARY CAHILL-BEKI WA ENGLAND AKIPAMBANA.
England iliingia kwenye mchezo huo, bila ya
wachezaji, Danny Welbeck ambaye huchezea Man U , Wayne Rooney na
mshambulizi wa Liverpool Daniel Sturridge ambao hawakucheza kutokana na
majeraha.
RICKY LAMBERT-MSHAMBULIAJI WA ENGLAND.
Uwezo wetu wa kushambulia ulikuwa mdogo sana kwa sababu hatukuwa na wachezaji, Rooney, Welbeck na Sturridge, alisema Hodgson.
"pia tulimpoteza kiungo cha kati, Alex
Oxlade-Chamberlain kwa sababu ya jeraha la goti ingawa wachezaji
waliowakilisha kwenye mchezo huo walicheza vyema.
STEVEN GERALD - NAHODHA WA ENGLAND
Sare hiyo iliisongesha England mbele kwa pointi moja kwenye kundi la H ikisalia na michuano miwili.
0 comments:
Chapisha Maoni