STRAIKA wa zamani wa Simba, Joseph Kaniki ‘Golota’ pamoja na
bondia chipukizi, Mkwanda Matumla wapo mikononi mwa polisi jijini Addis
Ababa, Ethiopia kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya.
Watuhumiwa hao wawili, raia wa Tanzania ambao
wanajuta na kububujikwa na machozi kila kukicha walifikishwa mahakamani
kwa mara ya kwanza Jumatatu iliyopita kwenye........
eneo linaloitwa Arada. Siku yoyote kuanzia leo Jumanne watapanda kizimbani tena kwa mara nyingine.
eneo linaloitwa Arada. Siku yoyote kuanzia leo Jumanne watapanda kizimbani tena kwa mara nyingine.
Mwanaspoti liliipata habari hii tangu Jumamosi
jioni na kuanza kuifanyia kazi kabla ya Kaimu Balozi wa Tanzania nchini
Ethiopia, Samuel Shelukindo kuithibitishia Mwanaspoti jana Jumatatu
kwamba wanamichezo hao wameshikiliwa nchini humo na polisi wa Kitengo
cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai.
Wanamichezo hao walikamatwa na kilo saba za dawa
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa, Mkwanda
akikutwa na kilo nne wakati Kaniki alikuwa na kilo tatu.
Walikuwa wanajiandaa kuunganisha ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia wakielekea Paris, Ufaransa.
“Wameshikiliwa hapa Ethiopia kwa zaidi ya siku 10
sasa, sisi tulipigiwa simu na polisi wa hapa Alhamisi kujulishwa kwamba
kuna Watanzania wawili wameshikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya
kulevya, tulipokwenda tukamkuta ni Kaniki na Matumla,” alisema
Shelukindo.
“Wao wenyewe wanaeleza kwamba walipitia Mombasa na
huo mzigo walipewa na mtu mmoja wao walikuwa hawaelewi ukoje. Lakini
Kaniki yeye anajitetea kwamba huyo aliyewapa huo mzigo pale Mombasa
anajuana vizuri na Mkwanda. Kwa hiyo alichofanya yeye ni kuubeba tu,
walikuwa wapite hapa Addis wakashuke Paris, Ufaransa ndio warudi Sweden
kwa njia zao wanazojua wenyewe. Walipofika hapa Mkwanda alifanikiwa
kupenya akapanda ndege lakini Kaniki akanaswa na mbwa ndipo akajitetea
kwa polisi kwamba lile begi lilikuwa lake lakini mizigo mingine ilikuwa
ya Mkwanda.
“Ndio hapo sasa Mkwanda akashushwa kwenye ndege
wakashikiliwa na Jumatatu ya wiki iliyopita wakapandishwa kwenye
Mahakama ya hapa kutajiwa kesi yao lakini hawakupewa nafasi ya
kujitetea, hiyo kesi itatajwa tena Jumanne (leo) na Jumatano (kesho) na
uchunguzi wa Polisi bado unaendelea.
“Kilichotokea ni jambo la aibu kwa nchi na hata
wachezaji wenyewe wanajuta kwa mfano Kaniki anasema alikuwa aende
England kucheza mpira mwezi Desemba lakini sisi tukamwambia hatuwezi
kumsaidia inabidi akabiliane na kesi iliyoko mbele yake. Mkwanda yeye
ametuambia kwamba anaishi Sweden hatuna maelezo yake zaidi,”alisema
Shelukindo na kuongeza kuwa wamewapelekea wanamichezo hao msaada wa
mablanketi kwa vile bado wako mahabusu na kwamba Ethiopia kwa sasa ni
baridi kali.
Shelukindo alisema kwamba wachezaji hao wanaishi
mahabusu kwenye kituo cha polisi (Federal Police Crime Investigation) na
hawana chochote zaidi ya nguo walizokuwa wamevaa.
Alisema kuwa uwezekano wa Kaniki na Matumla
kuachiwa au kesi yao kurudishwa Tanzania haupo kwa kuwa nchi hizi mbili
hazina utaratibu wa kubadilishana wafungwa.
Shelukindo alisema pia Watanzania wengine waliokumbwa na madai kama yao walihukumiwa nchini Ethiopia.
“Kuna Watanzania wengine walinaswa hapa miaka ya nyuma wao
walikuwa wamemeza wakapasuliwa yakatolewa na baadhi yao walifariki, hao
wanne ambao wamemaliza vifungo vyao vya miaka minne wanaweza kurudishwa
Tanzania muda wowote kuanzia sasa lakini kwa kesi kama hizi kifungo
chake kama wakikutwa na hatia inakuwa ni miaka tisa mpaka 15.”
Wanamichezo hao inasemekana walikabidhiwa mizigo
hiyo baada ya kupita sehemu zote za ukaguzi kwenye Uwanja wa Ndege wa
Mombasa, Kenya.
“Walipewa mizigo hiyo wakati wakifanya taratibu za
kupewa pasi ya kupandia ndege. Walipewa mizigo hiyo na huyo mtu na
wakagongewa mihuri na ndio wakaelekea kwenye ndege,” kiliongeza chanzo
chetu.
Mtu huyo aliwaomba wamsaidie kubeba mizigo ya dada
yake, ambaye anaishi Sweden. Wanamichezo hao waliwaeleza maofisa
ubalozi wa Tanzania huko Ethiopia kuwa hawakuwa wanafahamu kilichokuwemo
ndani ya begi hilo.
Hata hivyo, Shelukindo alisema mzigo huo ulikuwa umeshindiliwa chini kabisa ya mabegi yao
CHANZO NA MWANASPOTI.
CHANZO NA MWANASPOTI.
0 comments:
Chapisha Maoni