Searching...
Ijumaa, 9 Agosti 2013

ZANZIBAR WATUMA SALAAM ZA POLE KENYA KUFUATIA UWANJA WA NDEGE KUUNGUA MOTO


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Kenya Nchini Tanzania Balozi Mutinda Mutiso hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
 
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasilisha salamu za pole kwa Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Balozi Mutinda Mutiso kufuatia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa nchi hiyo kukumbwa na Moto.
Pembeni yao kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed.
Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mutinda Mutiso akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kamusi ya Kiingereza kwa Kiswahili aliyoitunga kwa ajili ya kukuza lugha hiyo pamoja na kusaidia wana diplomasia.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Balozi wa Kenya Nchini Tanzania anayemaliza muda wake wa utumishi wa miaka minne zawadi ya kasha kama kumbu kumbu ya kuwepo kwake Nchini.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!