Kocha wa Chelsea Jose Mourinho kwa mara ya kwanza ameonyesha hadharani wasi wasi wake juu ya mshambuliaji wake Fernando Torres kuhusu maisha yake ya baadae ndani ya klabu hiyo kwa kutamka hadharani kwamba Torres hana thamani ya paundi milioni 50 Roman Abrahamovic alizomnunulia kutoka Liverpool.
Akizungumza baada ya mechi kati ya Chelsea dhidi ya Manchester United mechi ambayo iliisha kwa sare ya o-o ambapo safu ya ushambuliaji ya Chelsea walionekana kuboronga Mourinho amelalamikia kiwango cha Torres akisema kiwango alichokionyesha katika mechi hiyo ni kidogo na hakilingani na thamani yake klabuni hapo ambapo alipoteza nafasi tano za kufunga.
‘hana thamani ya paundi milioni 50,labda milioni 20 au 25,’alisema Mourinho.
‘alifunga goli lililoipa ushindi Chelsea katika ligi ya klabu bingwa bingwa ulaya,pale alionyesha thamani kidogo ya mamilioni.
‘pia alifunga goli dhidi ya Everton ambalo lililoipeleka timu klabu bingwa ulaya,pale pia alionyesha thamani ya milioni kadhaa.
JOSE MOURINHO AKIMLALAMIKIA TORESS BAADA YA KUPOTEZA NAFASI YA KUFUNGA JANA.
Katika mechi ya jana Torres, Demba Ba na Romelu Lukaku walianzia bench ambapo Mourinho aliwaanzisha Eden
Hazard, Oscar, Kevin De Bruyne na Andre Schurrle.
Baada ya mechi ya jana Mourinho hakuficha matamanio yake ya kusajili washambuliaji wengine ambapo anatarajiwa kuelekeza nguvu zake kwa Samwel Etoo baada ya jitihada za kumn'goa Rooney Man U kuonekana kugonga mwamba,na wachambuzi wa masuala ya soka wanasema kutua kwa mshambuliaji yoyote Chelsea itamaanisha mwisho wa Torres au Demba Ba
0 comments:
Chapisha Maoni