Searching...
Ijumaa, 9 Agosti 2013

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YASIKITISHWA NA TUKIO LA KUMWAGIWA TINDIKALI WAZUNGU WAWILI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akielezea jinsi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilivyosikitishwa na Kitendo cha raia wawili wa Uingereza Katie Gee na Kisty Trup cha kumwagiwa tindikali { Acid } na watu wasiojuilikana katika maeneo ya Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk, Kulia yake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed Aboud Mohammed wakiambatana na Bamalozi wa heshima wa Uingereza, Ujerumani an Marekani waliopo hapa Zanzibar.
Kikao hicho cha dharura kilifanyika Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar na kushuhudia pia na baadhi ya Viongozi wa Jumuia za utembezaji watalii za hapa Zanzibar ZATO na ZATI.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!