Searching...
Jumamosi, 10 Agosti 2013

SAMWEL ETOO AONYESHWA MLANGO WA KUTOKEA ANZI,AAMBIWA ATAFUTE TIMU YA KUHAMIA NEWCASTLE,CHELSEA,NAPOLI NA GENOA WAMTOLEA MACHO



Newcastle offered shock Eto'o deal
SAMWELI ETOO.
Timu ya Newcastle United wameambiwa na klabu ya Anzhi Makchakala  kwamba wanaweza wakamchukua mkameroon huyo kwa bei ya kutupwa ikiwa ni moja ya mikakati yao ya kupunguza wachezaji wanaolipwa hela nyingi pasipo sababu.
Timu ya Anzhi iliishtua dunia pale walipotangaza dau la uhamisho la paundi milioni 17 wa kumsajili Samweli Etoo mwaka 2011 akitokea timu ya Inter Milan na kumlipa paundi 350,000 kwa wiki na kumfanya awe mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa kuliko yeyote duniani.
Klabu hiyo ya Urusi imetangaza kupunguza bajeti yake wiki hii kwa asilimia 60,mchezaji huyo raia wa Cameroon ameambiwa kwamba ni lazima atafute timu ya kuhamia msimu huu.
Tayari vilabu vya Italia vya Napoli na Genoa wameonyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo na sasa wapo kwenye maandalizi ya kukaa meza moja na  Anzhi ili kujadili uhamisho wa Etoo lakini wakala wake amesema anataka Etoo akacheze ligi kuu ya England msimu huuSoccer - Premier League Preview PackageJOE KINNER- NEWCASTLE

Ule usemi usemao ukisema cha nini wengine wanasema nitakipata lini ndio unadhihirika kwa Etoo kwani mara tu baada ya taarifa hizo kutolewa tayari vilabu vya Chelsea na Newcastle wameonyesha nia ya kumnasa mfumania nyavu huyo 
Bado Newcastle hawajakubaliana moja kwa moja na Anzi kuhusu uhamisho huo ila imeelezwa kwamba ada yake ni paundi milioni 5 na kama Etoo atakubali kutua St James’ Park basi akubaki kwamba mshahara wake utashuka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na huu aliokua akiupata huko urusi.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!