Searching...
Jumanne, 6 Agosti 2013

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI MBAYA SANA YA GARI MBEYA

GARI AINA YA TOYOTA COROLLA  ILIYOGONGANA NA BASI LA HOOD MENEO YA MSWISWI MBEYA DEREVA WA GARI NDOGO AMEFARIKI PAPO HAPO
HATI YA KUSAFIRIA YA MAREHEMU DAVIS HANAMUNDE MZAMBIA

MNAMO TAREHE 04.08.2013  MAJIRA YA SAA 06:45HRS HUKO MSWISWI WILAYA YA MBARALI BARABARA YA MBEYA/IRINGA, GARI NO T. 159 AXM AINA YA SCANIA BUS MALI YA KAMPUNI YA   HOOD LIKIENDESHWA NA DEREVA OMARY  SAID, MIAKA 50, MZIGUA, MKAZI WA MABIBO DSM LILIGONGANA NA GARI NO IT.3014 TOYOTA COROLLA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA DEVIS  ANAMUNDE, MIAKA 28, MZAMBIA MKAZI WA MUNZE LUSAKA NA KUSABABISHA KIFO CHA DEREVA HUYO PAPO HAPO.
 MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA MAGARI YOTE MAWILI NA DEREVA WA HOOD BUS AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHANA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
 Picha zote na Mbeya yetu Blog

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!