BENCHI LA UFUNDI LA CHELSEA LIKIONGOZWA NA MOURINHO AMBAO WAMEAPA KUPAMBANA MPAKA SIKU YA MWISHO KUMPATA ROONEY.
Jose Mourinho ameendelea kusisitiza kwamba atapambana mpaka siku ya mwisho ya usajili kuhakikisha anamsajili mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney.
Tayari Chelsea
wamegonga mwamba mara mbili lakini Mourinho amesema : "Bado muda upo wa kutosha katika hili".
HAPA ROONEY ALIKUA ANAELEKEA UWANJANI KWAAJILI YA MAZOEZI.
Rooney ameendelea kukasirishwa na kocha wa Man U Moyes baada ya jumnne wiki hii kuendesha gari lake In th hadi uwanja wa mazoezi lakini kocha hakumjumuisha na timu badala yake akamtaka akafanye mazoezi na timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 21.
HAPA ROONEY AKIREJEA NYUMBANI BAADA YA KUKATALIWA KUFANYA MAZOEZI NA TIMU YA WAKUBWA.
‘Tumesema kwamba ni mmoja kati ya wachezaji tunaowahitaji kuwa nao,tumefanya hivyo katika njia sahihi za kimaadili, na tutaendelea kusema na kufanya hivyo mpaka siku ya mwisho kwasababu tunafanya mambo kisheria na kihalali.
‘hakuna mahusiano ya moja kwa moja na mchezaji,hakuna mawasiliano-hakuna kabisa,lakini ngoja tuone kama mambo yanaweza yakabadilika"alikaririwa
David Moyes
David Moyes
Rooney ameshamuambia kocha David Moyes kwamba anahitaji kuondoka lakini timu imezidi kusisitiza kwamba Rooney hauzwi kokote na kwa kiasi chochote.
CESC FABREGAS.
Manchester United wana hasira na hawataki kumuuza Rooney baada ya chaguo lao la kwanza la kumnasa kiuongo wa Barcelona Cesc Fabregas kugonga mwamba baada ya jana mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania kuweka wazi kwamba hana mpango hata kidogo wa kuondoka Barcelona
ROY HODGSON-KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England Hodgson kwa mara nyingine tena amesema anamuhitaji Rooney kwenye kikosi chake lakini amemtaka mchezaji huyo atakapojiunga na kambi ya timu ya taifa asahau habari zote kuhusu uhamisho wake mara Chelsea mara Manchester United na badala yake aelekeze nguvu na akili yake katika kuisaidia timu ya taifa.
‘Ninatarajia ataweka pembeni matatizo yake binafsi kwasababu najua kwa mchezaji professional anakua na wasaidizi,kwahiyo yeye anatakiwa kuitumikia England kwa nguvu na akili zake zote na sio vinginevyo,’ alisema Hodgson baada ya kumjumuisha Rooney katika kikosi chake.
0 comments:
Chapisha Maoni