Wakati leo kipyenga cha ufunguzi wa ligi kuu England kikitarajiwa kupulizwa kama mwanzo wa kutafuta bingwa wa ligi hiyo hapo mwakani tayari Kocha wa Chelsea Mreno Jose Mourinho ameanza mbwe mbwe zake kwa kuwabeza wapinzani wake wakubwa katika mbio hizo
Manchester United na Manchester City kwa kusisitiza kwamba si lolote si chochote.
Amewaambia waaandishi wa habari kwamba katika kipindi cha miaka miwili iliyopita wamekua mabingwa wa ligi hiyo kwa misimu tofauti lakini sio mabingwa wa kweli
‘Miaka michache iliyopita timu bora ilikua ni timu bora ..alisema Mourinho.
‘mnafikiri Manchester United walishinda taji la ligi kuu kwasababu walikua ni timu bora?...sidhani!! aliendelea kuwazodoa Man United
‘ilikua ni mwaka mmoja tu kabla ambapo Manchester City walichukua ubingwa!! je walikua ni timu ya kushangaza? Sidhani!! Aliwaponda Manchester City
Mourinho amejisifia kwamba kwa kipindi alichokuwa Chelsea mwaka 2004/2005, alishinda ubingwa wa ligi kuu kwa rekodi ya pointi 9.
‘zamani mlikua na timu bora ya Arsenal ambapo waliwahi kuchukua ubingwa pasipo kufungwa mechi hata moja na sasa mnayo Chelsea yenye rekodi ya kushinda kwa pointi 95...haya ndiyo maajabu.
‘Mabingwa wa miaka ya nyuma walikua mabingwa wa kweli lakini hii misimu miwili ya mwisho..NOOOO!!(HAPANA)
Chelsea imetabiriwa kuwa itakua timu bora msimu huu na kushinda ubingwa wa ligi na Mourino na kikosi chake wataanza mbio hizo za ubingwa kesho jumapili Hull City
0 comments:
Chapisha Maoni