Searching...
Jumanne, 13 Agosti 2013

MAJANGA CCM-YAWASIMAMISHA UONGOZI MADIWANI WAKE 8 BUKOBA












BUKOBA, Tanzania
Chama Cha Mapinduzi (CCM)  mkoa wa Kagera kimeamua kuwatolea uvivu na kuamua kuwasimamisha uongozi madiwani wanne katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba.
Imeelezwa kwamba hatua hiyo imechukuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kagera kutokana na kudaiwa kupuuza maelekezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho 
Kikwete.  
Taarifa iliyotolewa na  Katibu wa CCM wa mkoa huo Avelin Mushi imesema kuwa uamuzi huo umekuja kutokana na chama kujali maslahi ya wananchi tofauti ya watu binafsi. Mushi amewataja madiwani hao nane kuwa  Yusuph Ngaiza (Kata ya Kashai) ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya Bukoba, Samwel Ruangisa (Kitendagulo) ambaye ni Meya mstaafu na Mkuu wa mkoa wa mkoa wa kwanza wa mkoa wa Kagera, Murungi Kichwabuta (Viti maalumu) Deusdedith Mutakyawa (Nyanga) Richard Gaspal (Miembeni)Alexander Ngalinda (Buhembe) ambaye pia alikuwa Naibu MeyaDauda Kalumuna (Ijuganyondo) na Robert Katunzi wa kata Hamugembe.  
Mushi amesema kuwa  kufukuzwa kwa madiwani hao ni kutokana na mgogoro ulidumu kwa muda mrefu juu ya mbunge na meya ambapo Rais Kikwete akiwa ziarani Kagera alitoa agizo la wanachama hao kutoendelea na mgogoro huo. Pia, amesema kuwa vikao vya chama vimekuwa vikiendelea kwa kufuata kanuni na taratibu kwa kuwaonya juu ya kuhujumu serikali ya CCM kwa kushirikiana na madiwani kambi ya upinzani kutotekeleza maendeleo ya wananchi lakini wahusika wote wamekuwa wakikaidi maagizo ya kuitwa kwenye vikao.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!