Hatimaye Willian baada ya kusaini rasmi mkataba wa kukipiga na matajiri wa London Chelsea hapo jana leo hii amekabidhiwa kibali chake cha kufanya kazi England na kisha ametoboa siri iliyosababisha yeye kuikataa Tottenham dakika za mwisho.
akizungumza kwa furaha Willian mwenye umri wa miaka 25 baada ya kusaini mkataba huo wa uhamisho wa paundi milioni 30 jana na leo kupata kibali cha kazi amesaini mkataba wa miaka mitano kukipiga Stamford Bridge ambapo atakua anakula mshahara wa on 100,000 kwa wiki.
akitoboa siri iliyompelekea kujiunga na Chelsea na kuikacha Tottenham dakika za mwisho baada ya kukamilisha vipimo amesema amefanya hivyo ili kukamilisha ndoto yake ya kujiunga na kocha machachari Jose Mourinho.
‘Ninayo raha kubwa sana kuwepo hapa, hii ilikua ni ndoto yangu ya siku nyingi kuwepo hapa,’alisema Willian kwa furaha.
‘Chelsea ni miongoni mwa timu bora duniani,na sasa ninachezea moja ya timu kubwa duniani chini ya kocha bora duniani,kwahiyo hii ni ndoto yangu ambayo leo hii imegeuka kuwa kweli,sasa ninaangalia mbele ’
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili ataongeza ushindani wa kugombea namba na wakali wengine wenye vipaji kama Juan Mata, Eden Hazard,
Andre Schurrle, Oscar, Kevin De Bruyne na Victor Moses
Willian atavaa jezi namba kwa kipindi chote atakapokuwepo Stamford Bridge.
0 comments:
Chapisha Maoni