Searching...
Jumatatu, 12 Agosti 2013

KUMBE ROONEY HAUMWI,AONEKANA AKIFANYA MAZOEZI MAZITO NA TIMU YAKE YA TAIFA

'Injured' Rooney returns to train with England WAYNE ROONEY NA JERMAIN DEFOE
Ndani ya saa 24 baada ya Wayne Rooney kukosa mechi ya Ngao ya hisani kati ya Manchester United dhidi ya Wigan leo hii asubuhi ameonekana akifanya mazoezi na timu yake ya taifa ya England,Rooney ametumia muda wake mwingi wa mapumziko baada ya ligi kwa malumbano na timu yake akihusishwa na taarifa za kutaka kutimka klabuni hapo na kutua kunako Chelsea.
Hata hivyo kocha wa Manchester United David Moyes kwamba mabingwa hao wa ligi kuu ya England maarufu kama Premier League hawana mpango wowote wa kumuuza mfumania nyavu huyo.
Rooney anahusishwa na kuwa na maumivu ya bega wiki chache zilizopita na kwamba hiyo ndiyo sababu ya yeye kuwa nje ya kikosi chake cha Man u lakini jambo la kushangaza ni pale alipoonekana leo akijifua vilivyo na mshambuliaji mwenzake wa Southampton  Rickie Lambert ambaye naye pia amejumuishwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Roy HodgsonBURTON-UPON-TRENT, ENGLAND - AUGUST 12:  Wayne Rooney and James Milner of England during a training session at St Georges Park on August 12, 2013 in Burton-upon-Trent, England.  (Photo by Alex Livesey/Getty Images)
Huyo juu kulia ndiye Rooney ambaye Manchester United wanadai kwamba ni majeruhi,hata hivyo Rooney amehusishwa na kutaka kutimkia Chelsea miezi kadhaa iliyopita lakini wachezaji wenzake Robin van Persie na Nemanja Vidic wamemtahadharisha mchezaji huyo wa zamani wa Everton kwamba atakua mjinga kuhama klabu inayotetea ubingwa wa ligi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 katika mechi yake ya mwisho aliyoichezea timu yake ya taifa alifunga katika mechi waliyoshinda magoli 2-1dhidi ya Brazil na kumfanya kocha wake Hodgson kuibuka na ushindi usiokua umetarajiwa.
Kinachosubiriwa sasa ni kuona kama Rooney atakua imara kwaajili ya kucheza mechi yao ya kirafiki dhidi ya Scotland kesho kutwa jumatano katika uwanja wa Wembley na mwisho kabisa watu wanasubiri kuona kama atapangwa kwenye mechi ya jumamosi dhidi ya Swansea mechi ya ufunguzi wa ligi kuu England..

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!