Jaji wa Mahakama Kuu Francis Mutungi,
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Mheshimiwa Jaji Francis S.K. Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya
Siasa.
Taarifa
iliyotolewa Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Agosti 5, 2013, na kutiwa
saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi
huo ulianza Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013.
Jaji
Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama
vya Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa mujibu
wa sheria.
Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu, DAR ES SALAAM.
0 comments:
Chapisha Maoni