Searching...
Jumatano, 28 Agosti 2013

ARSENE WENGER AENDELEA KUWEWESEKA,SASA ANAMTAKA JUAN MATA

Wenger wants special Juan at Arsenal
JUAN MATA-CHELSEA.
Kocha mkuu wa Arsenal Arsene Wenger ameendeleza siasa za danganya toto kwa mashabiki wake ambapo kila kukicha anaamka na usajili hewa ambapo sasa zikiwa zimesalia siku tatu tu dirisha la usajili kufungwa usiku wa kuamkia leo Mzee Wenger ameamka na ndoto za kumtaka mchezaji wa kiungo mshambuliaji wa Chelsea Juan Mata akitaka kumsajili Arsenal, huku akiwa na wasi wasi kama Chelsea watakubali kumuachia kiungo huyo kuhamia timu yoyote ya ligi kuu England.
Baba yake na Juan Mata ambaye pia ndio wakala wake alikuwepo uwanjani kuishuhudia Arsenal ikimenyana na timu ya Fenerbahce katika uwanja wa Emirates jana usiku. 
Hata hivyo Wenger amekataa kusema kama baba yake na Juan Mata alikuwa ni mgeni wa Gunners,lakini amesema anahitaji kumsajili Juan Mata na alitaka kumsajili tangu akiwa Valencia mwaka 2011 kabla ya kuzidiwa nguvu na chelsea.
Injured: Arsenal's Lukas Podolski (Picture: AFP/Getty Images)LUKAS PODOLSKI
Arsenal the Gunners wanataka kusajili mchezaji wa nafasi ya kiungo mshambuliaji baada ya kukubwa na majeruhi Lukas Podolski,Mikel Arteta na Abou Diaby katika mechi yao dhidi ya Fenerbahce ambayo waliibuka na ushindi wa mabao 2-0
Hata hivyo kocha mkuu wa Chelsea Jose Mourinho amesisitiza kwamba mchezaji huyo hauzwi

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!