Habari za kusikitisha ambazo zimetufikia hivi punde zinasema jumla ya watu 13 wamefariki dunia usiku wa kuamkia hii leo huku 11 wakijeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Hiace kutoka kijiji cha Ngogwa wilayani kahama kwenda ushirombo mkoani Shinyanga kugonga lori kwa nyuma usiku wa kuamkia hii leo.
akizungumza na MCHOME BLOG kaimu kamanda wa pilisi mkoani shinyanga kamishna msaidizi wa polisi KIHENYA KIHENYA amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva gari lililokuwa limewabeba abiria hao aina ya Toyota Hiace kuligonga kwa nyuma lori lililokuwa limepaki pembeni kidogo ya barabara ambalo lilikua limeharibika.
Watu watatu kati ya 11 waliojeruhiwa wapo mahututi katika hosiptali ya mkoa wa shinyanga na ni watu wanne tu waliotambuliwa kati ya 11 waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
MCHOME BLOG inawapa pole sana wale wote waliopatwa na msiba huu mzito na MWENYEZI
MUNGU AZILAZE MAHALA PEMA PEPONI ROHO ZA WALE WOTE WALIPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI HIYO.
MUNGU AZILAZE MAHALA PEMA PEPONI ROHO ZA WALE WOTE WALIPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI HIYO.
0 comments:
Chapisha Maoni