Waziri
wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akionesha picha ya kijana Leonard
Jeremiah Monyo ( Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za
madawa ya kulevya aina ya heroine.
Kijana Leonard Jeremiah Monyo ( Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya aina ya heroine.
JUHUDI za Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe
za kupambana na dawa za kulevya nchini Tanzana zimeanza kuzaa matunda
baada ya jana akiwa katika ukaguzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
Julius Nyerere kunaswa kijana akijaribu kupita na dawa za kulevya katika
uwanja huo.
Kwa kile kuoneshwa kukerwa na tabia hizo, Dk. Mwakyembe amempiga
picha kijana huyo ambaye ni rasta na pita yake itasambazwa maeneo
tofauti, huku kesi yake ikiendelea ya kupatikana na madawa hayo ya
kulevya.
Akizungumza na vyombo vya habari leo ofisini kwake jijini Dar es
Salaam, Dk. Mwakyembe alimtaja kijana aliyekamatwa jana kuwa ni Leonard
Jeremia Monyo (Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za
madawa ya kulevya aina ya heroin akitaka kusafiri nazo kuelekea misokoto
ya bangi 34 akiwa ameficha kwenye begi lake.
Alisema kijana huyo rasta alinaswa na mtambo wa kukagua mzigo baada
ya wakaguzi kuushuku mzigo wake hivyo kuamuru ukaguliwe ndipo alipokutwa
na madawa hayo haramu akijaribu kusafiri nayo kwa ndege.
![Badhi ya wanahabari wakimsikiliza Dk. Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vEMy9KuP1eGklT45Z8FCWV1MNhpgd2z0zTd20HYJIWb7YMHCrN9nyTbx5IKDynjsmnhZScd5iabN68O1VoHoOkaaOgxjA3Ovws66kiLYZXNXpvQG7h2xQHccfiEoE_IcryMjLLqCc=s0-d)
Alisema kijana huyo kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa
uchunguzi zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya
kukutwa na dawa hizo haramu. Alisema kwa kile kuoneshwa kukerwa na
vitendo hivyo na kuamua kwa dhati kupambana navyo wamempiga picha kijana
huyo na picha zake zitasambazwa maeneo mbalimbali ili aonekane na umma
kujua watua ambao wamekuwa wakilichafua taifa nje na ndani kutokana na
biashara hizo haramu.
Dk. Mwakyembe amesema atahakikisha anafuatilia kesi ya kijana huyo
hadi itakapoishia ili uona hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wahusika
na vitendo hivyo kukomeshwa. Alisema maofisa wakaguzi wa mizigo wawili
(wote wasichana) ambao walimnasa kijana huyo watazawadiwa na kupandishwa
daraja kutokana na kazi nzuri waliyoifanya.
“Jana tu baada ya ukaguzi wenzetu ambao wanaona kama tunafanya mzaha
jana tena wakapitisha mzigo wa madawa ya kulevya kiwanja cha ndege cha
Dar es Salaam, kwa sababu vijana wetu sasa wameamka na hawataki mchezo
wakamkamata kijana huyo…,” alisema.
“Picha yake itasambazwa kila sehemu…sidhani kama tunahitaji upelelezi
kwa sababu tumekukamata na dawa za kulevya. Mimi na viongozi wangu
kupitisha dawa za kulevya akikisha kuuhakikisha.
Alisema kijana huyo alikamatwa majira ya saa mbili na nusu usiku
akiwa anasafiri kwenda nchini Italia kwa kutumia ndege ya kampuni ya
Swissair. Alisema kwa sasa kila atakayekamatwa na dawa za kulevya picha
yake itasambazwa maeneo mbalimbali ya nchi ili watu hao wajulikane.
Alisema kwa sasa taratibu zinafanywa ili kuhakikisha mizigo ya abiria
wanaowasili kutoka nje ya nchi kuingia Tanzania nao mizigo ikaguliwe
ili kuwabaini wanaoingiza bidhaa hiyo haramu ichini pia. Aliongeza zoezi
hilo litafanyika katika viwanja vya ndege na bandarini kwa kila mizigo
inapowasili.
Alisema lengo ni kuhakikisha viwanja vya ndege vinakuwa salama na
kuacha kutumika vibaya na baadhi ya watu, jambo ambalo limeendelea
kulichafua taifa. Alisem kiwanja cha Dar es Salaam ni kizuri na kina
vifaa vya usalama vya kutosha ila mapungufu yaliyopo ni kwa baadhi ya
wafanyakazi ambao wanatumia vibaya madaraka yao.
Dk. Mwakyembe ameahidi kuwataja na kuweka picha zao hadharani watu
ambao wanajihusisha na madawa hayo ya kulevya. Amesema wanatarajia
kutaja majina ya Watanzania ambao hivi karibuni walinaswa na dawa za
kulevya nchini Afrika Kusini katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo.
Alisema Watanzania wengine wamekamatwa Hong Kong wakihusishwa na dawa
hizo na wanafuatilia pia picha na majina yao yatawekwa hadharani muda
wowote.
0 comments:
Chapisha Maoni