Zaidi ya Nymba sita zimechomwa moto eneo la kijiji cha Voda tarafa ya Mbwewe mkoani pwani baada ya gari moja aina ya fuso lililokuwa limebeba marola ya mitumba kupinduka katika eneo hilo kitendo kilichopelekea wanakijiji hao kuiba mizigo iliyokuwemo kwenye fuso hilo na kisha wenye mali kulazimika kufanya msako mkali na kuikuta mizigo yao katika nyumba hizo ambapo kila nyumba iliyokutwa na mizigo hiyo ilichomwa moto papo hapo.
akizungumza kutoka eneo la tukio kamanda wa polisi usalama barabarani Chalinze Afande Sule amesema jeshi la polisi liliwahi kufika katika eneo hilo na kuzima fujo hizo na kuepusha madhara zaidi.
kutokana na ajali hiyo maelfu ya abiria kutoka DSM,Morogoro kuelekea kanda ya kaskazini wamekwama kwa muda mrefu barabarani kusubiri gari maalumu la kuja kuliinua gari hilo na kuliondoa barabarani hapo ili kuyaruhusu magari mengine kupita kuendelea na safari zao.
kijiji cha Voda kipo mbele kidogo ya Mto wami ukitokea Chalinze na kinapakana na mkoa wa Tanga..
taaraifa zaidi na picha za ajali hiyo endelea kutembelea MCHOME BLOG
0 comments:
Chapisha Maoni