Helikopta
maalum iliyowabeba viongozi wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mh. Freeman
Mbowe pamoja na Mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika walipowasili
eneo la Mnada Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kufanya mkutano wa
hadhara wilayani humo leo mchana.
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la
Hai, Mh. Freeman Mbowe akizungumza na wakazi wa wilaya ya Sengerema Mkoa
wa Mwanza ambapo amewaasa kushiriki katika kutoa maoni ya Katiba Mpya
kwa kutumia mabaraza ili kuleta mabadiliko na mapinduzi nchini.
Mwananchi
wa Geita ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akitoa maoni
yake ya Katiba mbele ya wakazi na wafuasi wa Chadema ambapo wengi wao
wametaka Ushuru wa Masoko ufutwe pamoja na baadhi ya kinamama
kulalamikia shida ya Maji kwenye Wilaya yao.
Mbunge
wa Jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika akiteta jambo na mmoja wa viongozi
wa Chadema Hemedi Sabula wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo
mchana wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Pichani
juu na chini ni Umati wafuasi wa Chadema na wananchi wa Sengerema
waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa
Mnadi wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.
Picha juu na chini watoto nao waliojitokeza kusikiliza sera za Chadema kwenye mkutano huo leo.
Uwanja ukiwa umefurika wakazi wa Sengerema wakati wa mkutano wa hadhara wa Chadema.
0 comments:
Chapisha Maoni