MUONEKANO WA BASI LA TAQWA BAADA YA AJALI
BAADHI YA ABIRIA WALIONUSURIKA KIFO KATIKA AJALI HIYO WAKIWA HAWAAMINI KAMA WAMENUSURIKA
HAPA ABIRIA WAKISUBIRI MSAADA
PICHA JUU NA CHINI ZIKIONYESHA JINSI BASI HILO LILIVYOHARIBIKA BAADA YA AJALI
Na Emmanuel Lengwa, Mbeya.
WATU 11 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya Taqwa
walilokuwa wakisafiria kutoa Jijini Dar es Salaam kwenda Lubambashi nchini
Congo DRC kugongana uso kwa uso na lori aina ya Center wilayani Mbarali.
Ajali hiyo mbaya ilitokea juzi majira ya saa 2:00 usiku
katika mtelemko wa mlima Mambi katika barabara Kuu ya Mbeya –Iringa wilayani
Mbarali ikihusisha basi la Kampni ya Taqwa lenye namba za usajili T 396 AXZ na
lori aina ya Center lenye namba za usajili T 175 BRA.
Baadhi ya watu walikuwa ndani ya basi hilo walisema kuwa
wakati basi hilo likiwa kwenye mwendo mkali katika mteremko huo, lori aina ya
Center ambalo lilikuwa likipandisha lilijaribu kupita gari lingine lilikuwa
limesimama kando ya barabara, ndipo magari hayo yalipogongana uso kwa uso na
kusababisha basi hilo kupoteza mwelekeo na kupinduka mtaroni.
Getruda Kambale ambaye ni raia wa Congo, ni miongoni mwa
abiria walionusurika kwenye ajali hiyo ambaye alisema kuwa licha ya basi lao
kubondeka vibaya, hakuna mtu aliyepoteza maisha ingawa baadhi ya abiria
wameumia vibaya.
“Tunashukuru Mungu hakuna mtu amekufa hapa, lakini dereva
wetu ameumia vibaya wamemchukua na kumkimbiza Hospitali,” alisema Kambale.
Alisema wakati yeye akiwa amewa amechoka baada ya kusafiri
kwa siku mbili akitokea Nairobi, alishtikia basi likiyumba kasha akasikia
kishindo kikubwa na ndipo alijikuta akitolewa kwenye gari hilo kupitia
dirishani.
Daktari Msaidizi wa Hospitali ya Misheni Chimala, Peter Seif
Kigombola alisema kuwa hospitali hiyo imepokea majeruhi 11, kati yao 10
walikuwa ji abiria wa basi la Taqwa na mmoja alikuwa ni dereva wa lori aina ya
Center.
Alisema abiria hao tisa hali zao zinaendelea vizuri, lakini
wawili ambao ni dereva wa basin a kondakta wake hali zao ni mbaya na kuwa
wamepewa rufaa ya kwenda katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi.
Alisema kuwa dereva na kondakta wake walivunjika viungo
mbalimbali vya miili yao kama vile mikono na miguu na kupata majeraha mengine
kichwani, hali ambayo imesababisha hali zao kuwa mbaya.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa bado Jeshi la Polisi
linaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo pamoja na kukusanya taarifa za majeruhi na kuwa atatoa
taarifa ya ajali hiyo baadaye.
0 comments:
Chapisha Maoni