Searching...
Ijumaa, 26 Julai 2013

USAJILI ULAYA NI KAMA MIPASHO YA TAARABU..FABREGAS HAUZWI KWA GHARAMA YOYOTE-BARCELONA WAIAMBIA MAN U.

Barca deal Moyes final Fabregas blow
CESC FABREGAS - MCHEZAJI BARCELONA.
Katika kile kinachoonekana usajili wa ulaya kufanyika kwa kupitia vyombo vya habari kama mipasho ya taarabu ya Tanzania asubuhi ya leo Man U walituma ofa ya kumnasa Fabregas kupitia vyombo vya habari na jioni hii Barcelona wamewajibu Manchester United kwamba mchezaji wao Fabregas hauzwi kwa gharama yoyote ile kwa madai kwamba tatizo la Barcelona sio hela bali wachezaji bora.
A-League All-Stars v Manchester United
DAVID MOYES-KOCHA MAN U
kocha wa United David Moyes alijitapa kwamba anaongeza nguvu ya mazungumzo ya kuinasa saini ya Cesc lakini inaonekana mhispania huyo analazimika kuendelea kukipiga panapo Catalan 
JOSEP MARIA BARTOMEU-MAKAMU WA RAIS BARCELONA.
Makamu rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu ameiambia United waache kuhangaika na Cesc kwani hakuna kiwango chochote ambacho kitawashawishi kumuachia Fabregas
‘Haijalishi aina gani ya ofa kutoka Manchester United itakayotushawishi kumuachia Fabregas..Cesc hauzwi,tutaendelea kuwa naye,’ alikaririwa Bartomeu
‘kuna kiwango chochote cha pesa kitakachotufanya tumuachie?HAPANA. Ni mchezaji mkubwa,mwenye kiwango cha juu,haijalishi kama Manchester United wanamtaka. tunajivunia klabu kubwa kama Man United kumtaka mchezaji wetu,ni jambo la kujivunia.’

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!