CHRISTIAN RONALDO ENZI HIZO AKIWA MAN U.
David Moyes believes he can lure Cristiano Ronaldo back to Old Trafford (Picture: Getty)
Kocha wa Manchester United David Moyes ameamua kuingia vitano kamili baada ya kuandaa ofa ya paundi milioni 80 ambayo anaamini kwamba pamoja na utajiri wa Real Madrid lakini ofa hiyo itawatoa udenda na kumuachia mshambuliaji mwenye kiwango cha juu duniani Cristiano Ronaldo
kurejea nyumbani msimu huu.
DAVID MOYES-KOCHA MAN U
Tangu Moyes achukue mikoba ya Sir Alex Ferguson mwezi uliopita anajitahidi kuhakikisha anawapata wachezaji bora ili kuhimili mikiki mikiki ya ligi kuu England baada ya kuwakosa Thiago Alcantara na kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas japo taarifa za leo zinaonyesha huenda wakafanikiwa kumsainisha Fabregas
Moyes anahaha kusaka mshambuliaji mwingine bora wa kusaidiana na Van Persie baada ya Muingereza Wayne Rooney kuweka wazi kwamba anataka kuondoka Old Trafford msimu huu
0 comments:
Chapisha Maoni