WAYNE ROONEY .
Taarifa kutoka klabu ya Chelsea zinasema sasa nguvu zao zote wanazihamishia kwa mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney baada ya chaguo lao la kwanza Edinson Cavani kuingiliwa na PSG
ROBERT LEWANDOWSKI.
wakati huo huo taarifa zinasema pia Chelsea wanaongeza juhudi zao kumnasa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski kama chaguo lao la pili baada ya Rooney.
Chelsea wanasema mshahara kwao sio tatizo: Chelsea wanaweza wakampa Cavani paundi milioni 250,000 kwa wiki anaoutaka ila sio kwa ada hiyo ya uhamisho
EDISON CAVAN
Kati kati ni kocha wa man u Davis Moyes akiwa na wasaidizi wake ambaye anatarajiwa kukutana na Rooney muda wowote kuanzia sasa kumshawishi asiondoke Man U kabla timu hiyo haijaondoka kwenda kupiga kambi Asia na Australia kwa maandalizi ya msimu ujao.
Kocha wa chelsea mreno Jose Mourinho ambaye amerejea kuifundisha klabu hiyo kwa mara ya pili baada ya kuifundisha mara ya kwanza kwa mafanikio makubwa ameonyesha uwezekano mkubwa wa kumshawishi Rooney kutua Chelsea msimu ujao.
CARLO ANCELOTTI.
katika hali isiyotazamiwa Real Madrid nao wameingilia kati uhamisho wa Edison Cavan ambapo Carlo Ancelotti amesema Cavan ndio chaguo lake la kwanza na tayari amepewa go ahead na viongozi wa Madrid kumnunua msukuma ndinga huyo,kwahiyo sasa ni vita kati ya mabilionea MADRID vs PSG...nani ataibuka kidedea kumnasa Cavan????
EDISON CAVAN.
Huyu ndiye anayeonekana kuwa mfalme wa
soka na lulu katika kipindi hiki cha uhamisho wa wachezaji baada ya
kugombaniwa na vigogo vya soka barani ulaya.
Chelsea
sasa wamesema wanalazimika kuelekeza juhudi zao kwa washambuliaji Wayne
Rooney na Robert Lewandowski baada ya Paris Saint-Germain kupandia ofa
ya Chelsea na kuweka mezani kiasi cha paundi milioni 43 ili kumng'oa
mshambuliaji wa Napoli Edinson Cavani jana mchezaji ambaye alikuwa ndio
chaguo la kwanza la Mourinho darajani msimu ujao.
Roman
Abramovich hataki kuingia katika vita vya kumgombea mchezaji huyo
japokuwa mabingwa hao wa ufaransa wanaomilikiwa na mabilionea wa Qatar
wanayo shoti ya paundi milioni 11 kama watamnunua mruguay huyo
Abramovich
anakumbuka rekodi aliyoifanya ya uhamisho wa mshambuliaji wa liverpool
wakati huo Fernando
Torres aliyemnunua kwa kitita cha paundi milioni 50 Januari 2011
anahofia kupata hasara kama hiyo kwa Cavan ambaye ana umri wa miaka 26
0 comments:
Chapisha Maoni