Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho akiongea kwa msisitizo
Na Muhidin
Amri—Mbinga
MWENYEKITI
wa chama cha Mapinduzi(ccm)mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho, amepata pigo la kisiasa
kufuatia mgombea aliyempandikiza katika kinyang’anyiro cha nafasi ya mwenyekiti
wa Halmashauri ya wilaya ya mbinga Alan Mahai kushindwa vibaya katika nafasi
hiyo kwa kuambulia kura 13 tu licha ya jitihada kubwa zilizofanywa na
mwenyekiti huyo wa ccm mkoa.
Uchaguzi huo
uliofanyika hivi karibuni, katika ukumbi wa ccm wilayani hapa ulilazimika kurudiwa baada ya
ule uliotakiwa kufanyika wiki iliyopita kuvunjika kufuatia baadhi ya wanachama
wa chama hicho kutoridhika kwa kuenguliwa kwa jina la mmoja wa wagombea hao Allanus
Ngai ambaye ameonekana kupendwa na wanachama wengi hasa madiwani na hadi kuchoma
moto ofisi ya ccm wilaya ikiwa ni kutaka kufikisha hisia zao kwa viongozi .
Katika
uchaguzi wa juzi,dalili za kushindwa kwa Mahai
zilionekana mapema asubuhi pale baadhi ya wajumbe waliposikika
wakilitaja jina la Ngai kuwa ni mtu
anayefaa kuiongoza Halmashauri ya Mbinga kwa sasa na kukosoa utaratibu uliotumika na
kamati ya siasa ya mkoa wa Ruvuma wa
kulikata jina la Ngai hadi pale vyombo vya juu ndani ya chama vilipohamuru jina
ilo lirudishwe na kufanyika upya uchaguzi huo ili kunusuru kutokeo kwa vurugu.
Kuanguka
huko kwa Mahai ni kama pigo kwa mwenyekiti
wa Chama mkoa, kwani katika siku za hivi karibuni ameonekana kukosa tena
mvuto kwa wananchama wa chama hicho na kuanza kumnyooshea kidole juu ya
mienendo yake ikiwemo tabia ya maringo na dharau aliyonayo hasa baada ya kuchaguliwa kushika nafasi ya
juu katika mkoa.
Wakizungumza
na gazeti ili mjini Mbinga mara baada ya
uchaguzi huo,baadhi ya madiwani na wananchi mbalimbali waliofika eneo la uchaguzi walipongeza hatua ya kuchaguliwa
Ngai kuwa mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya wilaya hiyo na kukosoa sera za
mwenyekiti wao wa Chama Oddo Mwisho kutaka kuongoza tena Halmashauri yao kwa
kumpandikiza mtu, licha ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri mpya ya
Nyasa.
Mmoja wa
madiwani hao James Stuhati wa kata ya Litumbanyosi alisema madiwani wamefanya
kile walichokihitaji wananchi wa Mbinga kwani walishachoshwa na uongozi wa Mwisho
ambaye alikuwa kiburi na mtu mwenye majivuno na hata kwa madiwani wenzake
waliomuweka madarakani.
Kwa upande
mwingine baadhi ya wananchi hao walisema,kuanguka kwa Mahai ni ishara tosha
kuwa Chama cha Mapinduzi kinatakiwa kujiangalia upya na kuacha tabia iliyopitwa
na wakati ambapo viongozi uwachagulia wananchi mtu wa kumpigia kura hata kama
hana sifa.
Georg
Badomoja alisema,huu ni mwanzo mzuri sio ndani ya chama tu bali hata katika
kuinusuru Halmashauri yao kwani tayari walishakosa imani na baadhi ya watumishi
wake wakiwemo wakuu wa idara(mkurugenzi Shaibu Nnunduma)ambaye anatajwa kwa matumizi mabaya ya fedha za
Halmashauri hiyo ambayo inaongoza kiuchumi katika mkoa wa Ruvuma.
“kuchaguliwa
kwa huyu mzee Ngai,tuna matumaini makubwa ya fedha zetu za maendeleo,sisi wana
Mbinga tulishaanza kukata tama na viongozi waliokuwepo siku za nyuma,na tunaiomba serikali ituletee
mkaguzi kutoka ofisi ya CAG aje kuangalia kama mali zetu ziko salama”alisema(Kassian
nyandindi) mmoja wa mwananchi ambaye hakutaka kutaja jina lake.
0 comments:
Chapisha Maoni