Searching...
Alhamisi, 25 Julai 2013

KUMBUKUMBU YA MASHUJAA NI VITUKO VITUPU , KICHAA AMZIBUA MAKOFI AFANDE KISA MILIO YA RISASI.


kaimu  mkuu  wa mkoa  wa Iringa Gerald Guninita  ambae ni mkuu wa  wilaya ya  kilolo  akiweka ngao katika mnara  wa mashujaa wa  jimbo la Iringa  waliopoteza maisha katika  vita kati  ya mwaka 1939 -1945  ,kumbukumbu  zilizofanyika leo katika  bustani ya Manispaa ya  Iringa
 Askari mstaafu  SSGT Augustino Sambangi ambaye ni mwenyekiti  wa askari  wastaafu mkoa  wa  Iringa akitoa heshima  zake katika  mnara  huo leo
  Askari mstaafu  SSGT Augustino Sambangi ambae ni mwenyekiti  wa askari  wastaafu mkoa  wa  Iringa akiweka  upinde  katika  mnara  huo
 Askari  na  mgeni rasmi wakitoa heshima zao katika mnara  wa  kumbukumbu ya  mashujaa leo

 Mkuu  wa mgambo  mkoa  wa Iringa COl Sv Shayo  akiweka shime  katika mnala  huo
 Mwakilishi  wa  wananchi  wa mkoa  wa Iringa mzee  Said Mdota  akitoka katika  mnara  huo baada ya  kuweka shoka  la  kumbukumbu



 Wafanyakazi  wa Hospital ya  Rufaa ya  mkoa  wa Iringa  wakiwa  wamepanda  juu ya uzio  kushuhudia kabla ya  kutimua mbio kutokana na milio ya  risasi
 Askari  wa  (JWTZ)  wakipiga  risasi  hewani kutoa  heshima kwa mashujaa hao
 Heshima kwa mashujaa  waliopoteza maisha  katika vita 
KUMBUKUMBU ya  siku ya mashujaa iliyofanyika   katika  bustani ya Manispaa ya  Iringa kwa  mkoa wa Iringa  imezua hali ya  taharuki  kwa  wananchi  wa mji wa Iringa wakiwemo  wagonjwa.........
katika  Hospital ya  rufaa ya mkoa  wa Iringa kutokana na risasi zilizokuwa  zikipigwa na askari  wa jeshi la kujenga  Taifa (JKT) .
Mbali  ya  baadhi ya  wananchi wanaouguza  wagonjwa  wao katika  Hospital hiyo ya Rufaa ya  mkoa wa Iringa  pamoja na  wafanyabiashara  wa  soko  kuu la Manispaa ya  Iringa  kujikuta katika hali ya  taharuki  kubwa  kutokana na milio  hiyo ya  risasi  iliyopigwa zaidi ya mara  moja na  askari  hao kama  sehemu ya  kuwakumbuka  wenzao.
Bado  mmoja kati ya  askari  polisi wa  kiume ambae jina lake  halikuweza kupatikana mara moja  alijikuta  akivamiwa na jemba mmoja  ambae anasadikika  kuwa ni kichaa na kuchezea  kipigo kabla ya  kusaidiwa na mwanajeshi  wa  jeshi la kujenga  Taifa (JKT)
Kichaa huyo  aliruka  ukuta  wa uzio  wa bustani  ya Manispaa ya Iringa majira ya saa 2 asubuhi  wakati  askari  hao  wakiwa katika harakati  za maandalizi ya  maadhimisho hayo  na kumvaa askari  huyo na  kuanza  kumpa  kichapo kwa madai anayumbisha  mambo .
Hatua  hiyo  ilimafanya  askari  huyo kupigwa na butwaa huku akishindwa  kujua  sababu ya  kuvamiwa  tena  mbele ya  viongozi  mbali mbali  waliokuwa  jukwaa kuu   wakisubiri mgeni  rasmi  kuwasili  eneo  hilo.
Kitendo  cha  kichaa huyo  kumvaa askari  polisi  kilimfanya mmoja kati ya  askari  wa JKT  kuingilia kati na  kumkamata  kichaa huyo na  kumtuliza  kwa maneno matambu kwa kumtaka aende  polisi  kumfungulia kesi  polisi  huyo aliyedai  kuwa amemtapeli .
Mtandao huu ulipozungumza na baadhi ya  watu  wanadai  kuwa  kichaa huyo ameendelea  kusumbua  watu mbali mbali mjini Iringa na kuwa jana  alipata  kumpokonya  kijana mmoja Baiskel yake kwa madai kuwa ameiba kwake .
Kamanda  wa  polisi  wa mkoa  wa Iringa  Ramadhan Mungi  amedai  kuwa  taarifa za  kichaa huyo kufanya  vurugu mbali mbali mjini Iringa anazo na  kuwa ili  kuepuka kuleta  madhara  zaidi anafanyajiotihada za  kuwasiliana na mamlaka  husika  ili  kupelekwa  katika  Hospital  ya  vifaa Milembe kwa matibabu  zaidi 
Awali  akizunguza na  mtandao  huu  wa matukio  daima  juu ya kumbukumbu  hizo  kaimu mkuu wa mkoa  wa Iringa Bw Gerald Guninita ambae ni mkuu  wa wilaya ya  Kilolo  alisema kuwa  lengo la  kumbukumbu  hiyo ni  kuendelea kuenzi mchango  wa  wanajeshi  hao.
Hata  hivyo  alitaka  jamii  kuendelea kuenzi amani ya  Taifa  hili kwa  kuwafichua wale  wote  ambao  wapo kwa ajili ya kuhatarisha amani ya  Taifa.
Huku  wa upande  wake mwenyekiti wa  askari  wastaafu mkoa  wa Iringa SSGT Augustino Sambagi  akipongeza  jitihada za  amiri jeshi mkuu  Rais Jakaya Kikwete  kwa  kuendelea  kuongoza nchi katika hali ya amani  zaidi.
Pamoja na pongezi  hizo  bado  alitaka wanajeshi ambao  wamestaafu kazi  zao kuendelea  kuwa mfano mwema katika jamii na kuepuka  kujiingiza katika vikundi vya uharifu .
Mstahiki meya  wa Manispaa ya  Iringa Aman Mwamwindi akiwataka  wananchi  pamoja na  wanasiasa  kuendelea  kuenzi amani ya  Taifa  na  kukemea  tabia ya baadhi ya  wanasiasa  kupandikiza  chuki kwa  wananchi.
Wakati  huo  huo baadhi ya  wananchi  swanaouguza  wagonjwa  wao katika Hospital ya  Rufaa ya mkoa  wa Iringa  wameeleza  kusikitishwa kwao na hatua ya uongozi  wa  mkoa  wa Iringa  kushindwa  kutoa taarifa mapema kwa wananchi  kuhusu  zoezi la upigaji wa  risasi  hewani kama  kumbukumbu zao
Kwani  walidai  kuwa milio  hiyo ya  risasi za baridi zimewatia  hofu zaidi huku baadhi yao  wakitaka  kutimua  mbio kwa  hofu  wakihisi  kuvamiwa na kuwa ni vema kwa  wakati mwingine  kutoa taarifa  mapema ikiwa ni pamoja na tahadhari kwa  wananchi . 
MATUKIO DAIMA

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!