Searching...
Alhamisi, 25 Julai 2013

HATARIIIIIII...WASOMALI 17 WAKAMATWA MKOANI KILIMANJARO,POLISI WATUMIA RISASI ZA MOTO

NOVATUS MAKUNGA - MKUU WA WILAYA YA HAI MKOANI KILIMANJARO.
Jeshi la polisi mkoani kilimanjaro limewakamata wahamiaji haramu 17 kutoka nchini Somalia na Ethiopia walioingia nchini kinyume cha sheria na kukutwa wakiwa wamehifadhiwa kwenye nyumba ya mtu mmoja huko boma ng'ombe wilayani hai mkoani kilimanjaro.
Akizungumza na MCHOME BLOG mkuu wa wilaya ya Hai Bwana Novatus Makunga amesema
jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa wananchi wasamaria wema kuhusu uwepo wa wahamiaji hao haramu ndipo jeshi hilo lilipoanza uchunguzi wa haraka na kubaini kwamba ni kweli wapo na ndio wakaenda kuwakamata.
ameongeza kuwa jeshi la polisi lililazimika kutumia risasi za moto kwa kupiga hewani katika harakati za kuwakamata wasomali hao baada ya kutaka kukimbia punde tu walipowaona askari wakiizingira nyumba hiyo walimokuwemo.
Bwana Makunga ameonyesha masikitiko yake makubwa kuhusiana na watanzania wenye tabia ya kuwaingiza wageni haramu na kuwahifadhi majumbani mwao na kuwataka wananchi kuwa karibu na jeshi la polisi,viongozi wa serikali au vyombo vya habari ili kutoa taarifa haraka pale wanapobaini maovu kama hayo.
Hata hivyo watu hao hawakuweza kujulikana mara moja majina yao,walipitia wapi wala walikua wanakwenda wapi baada ya kukataa kuzungumza kwa madai kwamba hawajui kingereza wala kiswahili.
Katika harakati za kuhakikisha wanapambana na wimbi hilo la wahamiaji haramu serikali inafanya jitihada za kuhakikisha wananchi wanapewa elimu jamii ya kutosha ili kila mmoja kuwa mlinzi wa mipaka yetu.
jeshi la polisi linamshikilia mmiliki wa nyumba waliokuwepo wahamiaji hao pamoja na gari moja dogo ambalo lilikuwa linawapelekea chakula.
 

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!