WAKATI Wema Isaac Sepetu akiongeza idadi ya magari kwa kununua mkoko wa maana, zilipendwa wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemziba mdomo baada ya kununua eneo kubwa ambalo ndani yake kuna nyumba tatu, jirani na anapoishi Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006, Ijumaa Wikienda lina maelezo kamili.
Eneo alilonunua Diamond katika Mtaa wa Kaprikoni-Kijitonyama jijini Dar.
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni Mtaa wa Kaprikoni-Kijitonyama jijini Dar na kusababisha watu kupigwa na butwaa na kudai kuwa kweli ‘dogo’ ana jeuri ya fedha kwa kitendo hicho cha kununua karibia mtaa wote huo.

Diamond.
Akizungumza na gazeti, hili muda mfupi baada ya kukamilisha kila
kitu kuhusiana na ununuzi wa eneo hilo ambalo kwa mujibu wake anatarajia
kujenga jengo lenye ghorofa nne na nyumba za kawaida tatu, Diamond
alisema kuwa anajitahidi kuongeza idadi ya mijengo anayomiliki kwa kuwa
ndicho kitu cha thamani kuliko magari.
“Najua (nyumba) zitanisaidia endapo muziki wangu utakosa soko. Mimi
na mama yangu (Sanura Kassim ‘Sandra’) tuliishi kwa dhiki sana na sasa
kwa kipindi hiki ambacho Mungu ananisaidia na kuniwezesha kupata fedha
kwa wingi, siwezi kuishi maisha ya anasa ya kununua magari ya kifahari,”
alisema.
Katika hali iliyotafsiriwa kuwa ni kumtunishia msuli Wema, jamaa
alitupia maneno: “Mimi siyo kama hao wanaokimbilia kununua magari ya
kifahari ili mradi waonekane wako juu kifedha.
Eneo alilonunua Diamond anayemiliki nyumba zaidi ya tano Dar lipo mtaa wa nne kutoka anapoishi Wema.
Eneo alilonunua Diamond anayemiliki nyumba zaidi ya tano Dar lipo mtaa wa nne kutoka anapoishi Wema.
CHANZO NA GLOBAL PUBLISHER
0 comments:
Chapisha Maoni