Searching...
Jumanne, 11 Juni 2013

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII BALOZI KHAMIS KAGASHEKI AFUNGUA MKUTANO WA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA TANAPA MKOANI IRINGA‏

1a
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akifungua mkutano wa Shirika la Hifadhi za Mbuga za Taifa TANAPA na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu Wajibu wa vyombo vya habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za taifa unaofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo Ofisi za Manispaa ya Iringa, Balozi Kagasheki amewaasa wahariri wa vyombo vya habari kujadiliana kwa undani suala zima la kukomesha ujangili na jukumu la wanahabari katika mkakati huo wakishirikiana na serikali kwa ujumla kupitia taasisi za ulinzi katika mbuga za wanyama, amewataka wahariri kuwa wabunifu kwa kuandika makala na habari za kiuchunguzi ili kuibua mbinu hizo chafu na majangili ili kutokomeza ujangili huo na kupata ufumbuzi kamili wa changamoto hizo za ujangili, ameongeza kwamba wizara yake iko tayari kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wahariri na wadau mbalimbali yatakayofanikisha kupata ufumbuzi wa kutokomeza kabisa ujangili katika mbuga na pia amejiwekea utaratibu wa kukutana na waandishi wa habari kila mwezi atakutana na vyombo vya habari ili kuzungumza na wanahabari kuhusu masuala mbalimbali ya wizara hiyo. 2a
  5a
1
Waziri wa Malisili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma wakati akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Siasa na Kilimo mkoani Iringa ambako mkutano wa Wahariri wa vyombo vya habari na Shirika la Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA unafanyika. 3
Mkurugenzi wa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akizungumza katika mkutano huo kukaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo unafofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo mjini Iringa
6A
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa Siana na Kilimo Mkoani Iringa 

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!