Wafanyakazi wa Kampuni
ya simu Tanzania (TTCL), wakifanya usafi wa
mazingira katika bustani ya hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es
Salaam, jirani na MOI ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya
Mazingira
Duniani.
Wafanyakazi wakifanya usafi katika lango kuu la hospitali ya
Taifa Muhimbili wakiongozwa na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu, Jotham Lujara.
Wafanyakazi wa TTCL wakiendela na usafi.
Kamimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Jotham Lujara (kulia) akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Makwaiya Makani wakati wa kileke cha maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani.
Picha ya pamoja.
HOSPITALI ya
Taifa Muhimbili (MNH) inatarajia kutoa huduma ya matibabu kwa njia ya mtandao
‘Tele medicine’ kwa kutumia mkongo wa taifa wa mawasiliano ili kupunguza gharama za kufuata matibabu nje
ya nchi.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari jana mara baada ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kufanya
usafi katika Hosptali ya Taifa ya (MNH). Ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya
mazingira duniani,Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya simu Nchini (TTCL),Jotham
Lujara alisema lengo la kufanya hivyo ni kupunguza gharama za kufuata matibabu
nje ya nchi kama vile India,Uingereza,Ujerumani na Afrika Kusini.
Alisema
hospital za KCMC na Bugando zimeunganishwa na TTCL na zimeshaanza kutoa huduma
ya matibabu mtandao kupitia huduma ya ‘fibre’ TTCL ambayo ni teknolojia ya
mawasiliano ya kisasa yenye ubora na viwango vya juu.
“TTCL kwa
kushirikiana na MNH na hospitali ya Amana wanaweza wakaanza kutoa huduma za
matibabu mtandao kama wanavyofanya hospitali ya KCMC,ambapo huduma hizi ni
mkombozi wa wanyonge zinakwamishwa na watu wanahujumu miundombinu yake kwa
kukata nyaya zinazopitisha pamoja na kukata mkongo wa taifa wa
mawasiliano,”Lujara.
Hata hivyo
alisema wanatoa wito kwa wananchi na jamii kwa ujumla kuwa na mazoea ya kufanya
usafi katika sehemu wanazoishi na sehemu zinazowazunguka kuepuka kutupa taka
hovyo na wahakikishe wanatupa taka kwenye vyombo husika.
Alisema kama
kauli mbiu inavyosema TTCL huleta watu karibu ndio maana wameamua kushiriki
katika siku hiyo kwa kufanya usafi Mnh
na kutoa hamasa kwa watu na jamii kwa ujumla kuona umuhimu wa kutunza mazingira
katika sehemu wanazoishi na sehemu zinazowazunguka.
Naye Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa MNH Makwaiya Makani
alisema anashukuru kwa kujiunga na TTCL
na kwa sasa wamo katika mchakato wa mwisho kuanza kutoa huduma hiyo.
Alisema pia
wanaishukuru kampuni hiyo kwa kuwapatia vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh.
milioni 1.5 huku akieleza jinsi
hospitali hiyo inavyohitaji kufanyiwa usafi mara kwa mara kwa kuwa kwa siku
wanaingia watu zaidi ya 2000 kuona wagonjwa wao.
0 comments:
Chapisha Maoni