Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya
ya Mbinga Anastasia Amasi akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambao hawapo pichani
Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya
ya Mbinga Anastasia Amasi akionyesha sehemu iliyoanzia moto kuwaka na kukamata pazia.
Kama unavyoona katika picha hapo ni ndani ya ofisi baada ya moto kuwaka
Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya
ya Mbinga Anastasia Amasi anayeonekana katika picha akitoa maelezo kwa nje ambapo walimwaga mafuta aina ya petroli dilishani na kuwasha moto
Huu ni mlango uliomwagiwa mafuta katika upenyo kisha
kuwashamoto ambao haukuleta madhara kama walivyo kusudiwa na wachomaji.
------------------------------
WATU wasiojulikana wamechoma moto jengo la ofisi ya Chama
cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma tukio lililotokea Juni 21 mwaka
huu majira ya usiku pamoja mlinzi wa ofisi hizo kuwepo katika eneo hilo la
ofisi mpaka majira ya saa 12 asubhi na
hakuweza kutambua kutokea kwa kitendo hicho kilichofanywa na watu wasiojulikana
usiku huo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo katibu wa chama cha
Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi amesema kuwa tukio hilo lilitokea
usiku wa kuamkia Juni 21 mwaka huu ambapo watu wasiojulikana walichoma moto
moja ya jengo la ofisi za chama hicho wilayani humo moto ambao ulielekelezwa katika chumba cha
ofisi ya katibu ambapo walivunja vioo na kuchoma moto mapazia lakini kabla
hawajachoma vitu vilivyokuwemo ndani walikimbia na kuacha dumu lililokutwa
likiwa na mafuta aina ya petrol
Alisema kuwa mpaka sasa hakuna hisia zozote zinazohusiana na
tukio hilo ingawa uongozi wa chama cha mapinduzi wilayani humo umeshatoa
taarifa kwenye vyombo ya ulinzi na usalama ambavyo vinaendelea na uchunguzi wa
tukio hilo.
Katika hatua nyingine hali ya sintofahamu imejitokeza katika
uchaguzi wa viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga baada ya halmashauri
hiyo kugawanywa na kuzaliwa kwa halmashauri mpya ya wilaya Nyasa kwa kuibuka
kwa vitendo vya hujuma vinavyodaiwa kufanywa dhidi ya mgombea mmoja wa nafasi ya mwenyekiti jina
lake kuenguliwa katika mazingira ya kutatanisha na kuzua maswali mengi miongoni
mwa madiwani wa halmashauri pamoja na wananchi na kutaka uchaguzi huo
usifanyike mpaka majina yote matatu ya wagombea yawepo.
Mmoja wa wananchi wa halmashauri hiyo ya wilaya ya Mbinga
ambaye pia ni katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi wa kata ya Mbinga mjini Monika John alisema
kuwa hizo ni dalili za kuwepo kwa njama za wazi za kupanga safu ya uongozi
ambao siyo chaguo la walio wengi bali ni chaguo la baadhi ya viongozi wa
halmashauri hiyo kwa masilahi yao.
Akizungumzia hali hiyo katibu wa chama cha mapinduzi wilaya
ya Mbinga alisema kuwa uteuzi wa wagombea wa nafasi hizo hufanywa kwa
kuzingatia kanuni za chama na wenye jukumu la mwisho la uteuzi ni uongozi wa chama ngazi ya
mkoa na yeye si msemaji wa maamuzi ya
ngazi mkoa ingawa amepokea tarifa ya kusitishwa kwa uchaguzi huo mpaka taarifa
nyingine itakapotolewa na ofisi ya chama ngazi ya mkoa.
0 comments:
Chapisha Maoni