Wayne Rooney wiki ijayo anatarajiwa kukutana na kocha wake mpya DAVD MOYES kujadiliana kuhusu hatma yake ndani ya klabu yake ya MANCHESTER UNITED
Taarifa zinasema Rooney bado ana hasira kufuatia kauli iliyotolewa na aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Sir Alex
Ferguson maarufu kama babu kufuatia kauli yake kwa umma kwamba anataka kuihama klabu hiyo msimu ujao kauli ambayo ROONEY amesema sio ya kweli na anachokihitaji ni kocha mpya MOYES kukiri kwa umma kwamba kauli iliyotolewa na babu FEGIE sio ya kweli vinginevyo lazima aondoke
wakati huo huo makocha wa Chelsea na Arsenal tayari wameshatangaza ofa nono ya kumng'oa Man U na taarifa za ndani kabisa zinasema ROONEY atatimiza ndoto yake ya muda mrefu kama atatua CHELSEA kwani MOURINHO ni mmoja kati ya makocha anaowahusudu duniani japo inaonekana MAN U hawapo tayari kumuuza kwenye klabu ambayo itashindana naye kuchukua kombe la ligi kuu England msimu ujao.
0 comments:
Chapisha Maoni