Mbunge
wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), akihutubia katika mkutano wa
hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Azimio, Tandika, Dar es Salaam,
mwishoni mwa wiki. Mtemvu alivikabidhi vikundi vitano vya Kuweka na
Kukopa (VICOBA, kila kimoja msaada wa sh. 500,000 na kikundi cha ulinzi
shsirikishi sh. 500,000 za kutunisha mifuko hiyo.
Mbunge
wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia), akikumbatiana na mmoja wa
wanachama wa kikundi cha Vicoba cha Tuyangatane waliofurahi kupatiwa
msaada wa sh. 500,000 za kutunisha mfuko wa kikundi hicho.
Wanachama wa Tuyangatane wakifurahia kupata hundi hiyo.
Mtemvu akikipatia kikundi cha Vigoba cha Tumaini msaada wa sh. laki tano
Kikundi cha Tupendane kikipatiwa laki tano
Mbunge
wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), kulia, akimkabidhi hundi ya sh.
500,000 Mweka Hazina wa Kikundi cha Saccos cha Pambazuko, Sophia Said,
kwa ajili ya kutunisha mfuko wao, katika mkutano wa hadhara uliofanyika
Uwanja wa Shule ya Azimio, Tandika, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Mtemvu alivipatia pia kiasi kama hicho vikundi vingine vitano.
Mtemvu
akimvisha filimbi Juma Mlanzi ambaye ni miongoni mwa walinzi
shirikishi 56 waliohitimu mafunzi ya kijeshi. Pia walikabidhiwa vyeti.
Juma Kambona akikabidhiwa cheti baada ya kuhitimu mafunzo hayo
Mbunge
wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), wa pili kulia, akimpatia cheti
Mwanaisha Gea ambaye amekuwa miongoni mwa vijana 56 waliohitimu mafunzo
ya Ulinzi Shirikishi, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa
Shule ya Azimio, Tandika, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Mtemvu
alikikabidhi pia kikundi hicho cha Ulinzi Shirikishi sh. 500,000 za
kuanzishia Saccos yao. Kulia ni Diwani wa Kata ya Azimio, Hamis Mzuzuri.
Jumanne Jumbe naye akikabidhiwa cheti baada ya kuhitimu mafunzo hayo
Mma
Mkazi wa Kata ya Azimio akilalamika mbele ya Mtemvu, kuhusu mchezo wa
Kangha Mbendembende au kangamoko unavyowadhalilidha wanawake ambapo
aliomba upigwe marufuku kwa vile auendani na maadili ya kitanzania.
Mgambo
Said Amiri akilalamikia kitendo cha mabosi wake wa Kituo cha Polisi cha
Tambuka Reli kinavyowalea vibaka na majambazi katika eneo hilo
.PICHA
ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
0 comments:
Chapisha Maoni