MREMBO aliyejulikana kwa jina la Pepetua Maina au maarufu kama
Lucy, Mkikuyu wa Kenya anayekadiriwa kuwa na miaka 25 mpaka 30 amekutwa
amekufa kwa kuchinjwa shingo na mwili wake kutupwa katika shimo la taka.
Mwili wa huo ulikutwa na polisi Juni 8, mwaka huu Mikocheni B,
jirani kabisa na makazi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Kamishna Suleiman Kova.
Kwa mujibu wa mtoa habari, mwili wa msichana huyo ulionekana na mfanyakazi mmoja wa ndani wakati akienda kutupa takataka eneo hilo ambapo alipouona alipiga kelele zilizowafanya majirani kukimbilia eneo la tukio na kujionea wenyewe.
Taarifa za kipolisi zilidai kuwa mrembo huyo kabla ya kuchinjwa
alipigwa kwani mkono mmoja wa kushoto ulivunjika na kukutwa na jeraha
kubwa katika paji la uso.
Wakizungumza na Uwazi kwa tahadhari kubwa kuogopa ushahidi, baadhi ya majirani wa eneo hilo walisema hawakusikia vurugu zozote usiku kwa hiyo huenda wauaji walimchinja mbali na kwenda kuutupa mwili wake eneo hilo.
Juni 9, mwaka huu, Uwazi lilizungumza na Kamanda wa Mkoa wa
Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Camillius Wambura kuhusu kifo cha
msichana huyo ambapo alikiri kutokea.
Kamanda Wambura alisema kuwa, Pepetua alikuwa akifanya kazi kwa Jaji Engera Kileo kwa miaka mitatu mpaka siku ya kifo chake.
Kamanda Wambura alisema kuwa, Pepetua alikuwa akifanya kazi kwa Jaji Engera Kileo kwa miaka mitatu mpaka siku ya kifo chake.
“Jeshi la polisi tulipokea habari za kuwepo kwa mwili huo jana
(Jumamosi) saa sita na nusu, tukaenda na kuukuta ukiwa kwenye shimo la
taka umechinjwa shingoni na kiganja cha kushoto kilikatwa na kitu chenye
ncha kali na kwenye paji la uso alipasuliwa.
“Tuliuchukua na kwenda kuuhifadhi Hospitali ya Mwananyamala. Vijana
wawili wanaoishi kwa Jaji Kileo ndiyo waliofika hospitali na kumtambua
marehemu. Jaji mwenyewe alikuwa safarini nje ya nchi, amerejea leo (juzi
Jumapili).
“Mpaka sasa tunamshikilia mtu mmoja kwa mahojiano kuhusiana na kifo
hicho, siwezi kuzungumza kwa undani zaidi,” alisema Afande Wambura.
SOURCE:hi255 (138)
0 comments:
Chapisha Maoni